Ukisema Jini tayari kuna majini miatatu karibu yako. Kila mtoto mchanga huguswa na jini dakika moja bada ya kuzaliwa. Vitabu vya dini vinasemaje?

Mkuu! Naomba nikurekebishe hapa unaposema majini yanakufa unakuwa unakosea sana simply because hawa majini ni roho na hawana mwili na siku zote kinachokufa ni kile chenye umbo, maada au (matter) na chenye umbo pekee ni binadamu ndio maana tunakufa ila majini na malaika wameundwa kwa space and time bila kuwa na umbo maalumu wale ni spiritual energy pekee na laws of nature zinasema energy can neither be created nor destroyed it can only be transformed or transferred, hivyo unaposema majini wanakufa unakuwa unakosea wale wana roho tu na hawana miili sasa wanakufaje ilhali wao ni roho tu?

Malaika, majini hawa ndio pekee Mungu aliwapendelea na kuwapa roho pekee kama vile yeye alivyo ila sisi binadamu ndio tukapewa mwili, roho na nafsi.. Sasa tunakiona cha mtema kuni kwenye huu mwili uliobeba deni la Dunia almaarufu kama tumbo usipochakarika kutafuta maisha unahadhirika mchana kweupe tu.

Majini ni immortal ila binadamu ni mortal being.
 
Ukisoma vema kuhusu majini utaona kabisa ni viumbe wanaokufa kwa sababu wameumbwa na mungu na kiumbe chochote kinachozaliana lazima kife,ukisema hawafi unamaanisha hawazaliani,pia ukisema hawafi inamaana mungu aliwapa uwezo sawa na wake na Kama ndivyo wasingeliweza kuishi kwa kuogopa neno la mungu mana hawafi hivyo hata kuwakemea wsingelikimbia mana hawafi na mungu Hana uwezo wa kuwaua.
Jini anakufa ila anaishi miaka kuanzia 400 na kuendelea na hii ni kwa sababu hana umbo maalumu......

Elimu hii ni pana sana na kwa sababu ya muda ndio maana niliishia hapo Chief ila ahsante kwa elimu yako pia hakika tunajifunza sote
 
Mkuu, wanakufaje wakati wao ni roho pekee? Wao wana sifa nyingi sana zinazofanana na malaika tu, ishu ni kwamba wao ni malaika waliohasi ufalme na neno la Mungu.

Hizi story za hizi njemba jini kufa ni hadithi tu za kusadikika hazina ukweli wowote. Majini ni roho na roho haijawahi kufa bali mwili hufa.

For a simple reason ya wao kuishi rohoni, hivyo hawafi Mkuu. Asante.
 
Mkuu jini sio malaika muasi ila wanaongozwa na malaika muasi tena mwenye cheo cha tatu,jini anaumbo lake kamli ila anao uwezo wa kujibadilisha atakavyo,ukisema jini ni hadithi inamaana hata mungu utasema ni hadithi,
Hawa viumbe utasema pia hawazaliani au utasemaje?!
Hawa ni viumbe wa mungu waliopata kuishi duniani kabla ya mwanadamu hajaumbwa kureplace uwepo wao....
Natamani tujadili kiupana zaidi ila sina muda kwa sasa na pia ninapojifunxa au kutaka kujifunza zaidi huwa naogopa sana watu wanaohitimisha kitu kwa kusema neno HADITHI mana hana jipya la kuweza kusaidina kuchanganua jambo

Hivyo basi niseme wewe ndie unahadithi za kusema jini ni roho wakati sio kweli jini sio roho jini ni kiumbe anaeishi nje ya uwezo wa mwanadamu kupata kumshuhudia na hii ni adhabu ya mungu juu yao baada ya kusema mwanadamu akiumbwa basi wao watamuua (soma vizuri biblia ama Quran)
Lakini pia soma kuhusu mfalme Suleiman alieishi na kuwaongoza majini hadi kifo chake na walimsaidia kujenga mahekalu kadhaa je roho inaeeza fanya kazi za kibinadamu mana roho ni kama upepo tu hauonekani na hauna umbo.

Soma vitabu vingi uwezavyo na utaachana na neno HADITHI
 
Tusidanganyane hapa mkuu, hakuna tofauti kati ya Majini na Mashetani, wote ni hao hao tu. Hakuna tofauti kati ya Mapepo na Maruhani. Kwa kifupi ni kwamba malaika wote walioasi Mbinguni na kufukuzwa ndiyo hao leo hii wanaitwa majina tofauti tofauti, wengine wanawaita Majini, Mapepo, Mashetani, Vibwengo, Maruhani, Mizimu, Mazimwi, Mapopobawa n.k.

Hawa wote ni malaika walioasi Mbinguni na kiongozi wao ni mmoja tu ndiye Lusiferi. Huyu Lusiferi moja ya mbinu yake ni kuwachanganya Wanadamu akili zao kwa kuwadanganya kuwa kuna tofauti kati ya Majini na Mashetani. Kwa kifupi tu ni kwamba Lusiferi amekuja na majina ya aina mbali mbali ambayo amewapa wale malaika waliomfuata ili kuwapoteza Wanadamu waone kuna tofauti kumbe kitu ni kile kile!

Mbinu hii ya Lusiferi inaitwa "divide and rule" yaani "watenganishe na uwatawale". Lusiferi amewatenganisha hawa malaika wake kwa kuwapatia majina tofauti tofauti ili waweze kuwatawala Wanadamu kirahisi na hilo wamefanikiwa sana kwani leo hii kuna Mamilioni ya Wanadamu wanaamini kuna Majini wazuri na Majini mabaya. Leo hii Wanadamu wanaamini kuna Mizimu na Mashetani.

Tena Lusiferi amefanikiwa sana kuwatenganisha Wanadamu pia, YESU alipokuja na Mafundisho ya INJILI, Lusiferi akaja na QUARAN(Waislamu mtanisamehe kwani huo ndiyo UKWELI ulivyo). Tena ndani ya Ukristo Lusiferi amefanikiwa kuwagawa sana kwani kuna waabudu JUMAPILI na waabudu siku ya JUMAMOSI, kote huko amevuruga vuruga ili kuwatenganisha. Lipo kundi dogo sana linaloshika mafundisho ya KWELI ya MUNGU linaitwa KANISA LA MUNGU.

Hili nalo Lusiferi amefanikiwa kulivuruga mno kiasi limegawanyika sana na kamebakia kakikundi kadogo sana kanakoshikilia Amri za MUNGU na Imani ya KWELI ya YESU. Hii yote ni ili yatimie yale maneno ya YESU kuwa watakaokolewa ni KUNDI DOGO SANA!

UKWELI ni kwamba hakuna tofauti yoyote ile kati ya hao viumbe niliowataja, wote hao ni wale malaika walioasi Mbinguni na kuja duniani wakimfuata Lusiferi, wote ni kitu kimoja na tabia zao ni moja isipokuwa tu wanajifanya kuwa tofauti ili kuwapotosha Wanadamu na kuwadanganya.

Ndiyo maana Yesu alisema itafuteni KWELI nayo hiyo KWELI itawaweka huru kweli kweli. Mwenye masikio na asikie!

Cc. Kudo Da'Vinci Mshana Jr zitto junior Che mittoga Tz mbongo Sky Eclat Otorong'ong'o SALA NA KAZI mitale na midimu Dejavu Shubiri Pori nyabhingi Mr Q
 
Ni kundi gani hilo litakalo okolewa pekee?
 
Mkuu sijataka watu waamini uzuri wa jini au ubaya wake ila nilileta mada tujifunze pamoja bila kuingilia muhimili wa dini zetu

Lakini naomba nikuulize ni malaika wangapi walimwasi mungu?! Na kwanini katika wingi huo ulioutaja ila Bible inamtaja Lucifer kama ndie malaika alie muhasi Mungu na si hao makabila 72 elfu wa majini?!

Je unaamini kwamba shetani ni kiumbe yeyote mwenye kufanya yasiopendeza akiwemo mwanadamu?!

Sijajua lengo lako ni nini hasa mana mada imeeleza maisha ya viumbe hao na si wema ama ubaya wao na bado nimeonesha njia za kukukabiliana nao lakini pia hat
 
Lakini naomba nikuulize ni malaika wangapi walimwasi mungu?! Na kwanini katika wingi huo ulioutaja ila Bible inamtaja Lucifer kama ndie malaika alie muhasi Mungu na si hao makabila 72 elfu wa majini?!
Mkuu malaika waliomuasi MUNGU kwa idadi yao ni theluthi ya malaika wote na kiongozi wao ni Lusiferi(UFUNUO 12:3-4). Alianza Lusiferi kuasi na akaweza kuwashawishi theluthi ya malaika wengine nao pia wakaasi. Hakuna tofauti yoyote ile ya malaika waasi na majini, hao ni kitu hicho hicho kimoja.

Malaika hawa walioasi pamoja na Lusiferi mwenyewe ndiyo hao wanaitwa mashetani, maana ya "shetani" ni "adui" au tunaweza kusema ni "adui ya MUNGU". Kwa udanganyifu wa Shetani amewadanganya na kuwafanya muamini kuna tofauti kati ya shetani na jini, wakati ukweli ni kwamba hakuna tofauti yoyote ile, shetani ndiyo huyo huyo jini na jini ndiyo huyo huyo shetani.
 
Nataka unitajie wewe ni kundi gani/linaitwaje?
Wewe na elimu yako yote ya "Theology" hulijui kundi la KWELI la MUNGU?? Theology uliyosoma inakusaidia nini mkuu? Kweli sasa nimeamini maarifa ya Wanadamu ni upumbavu mbele ya MUNGU(1 WAKORINTHO 3:19-20).

Mkuu kama unataka kuunganishwa na hilo Kanisa la kweli la MUNGU basi wewe zishike Amri zote za MUNGU na imani ya YESU KRISTO kisha Roho Mtakatifu atakuongoza kwenye hilo kanisa. Imeandikwa hakuna anayekuja kwa BABA pasipo kuvutwa na Baba(YOHANA 6:44). Pia YESU alisema yeye atakayenipenda na kuzishika Amri zangu, tutakuja kwake na kufanya makao kwake(YOHANA 14:23-24).
 
Mkuu mimi nimeshika sheria zake zote Mungu (hua nazivunja muda mwingine coz sijakamilika) nafuata mafunzo ya Yesu kristo je nimeunganishwa na hilo kanisa?
 
Nilitegemea nitaona kanisa la kule Ileje Mbeya kumbe bado unaleta story za kimishionari kwamba Africa hakuna Mungu?

Sijui waafrika sisi tuna kazi gani hapa Duniani kama hata Mungu mwenyewe hatutambui!
Mkuu nani kakuambia NENO la MUNGU limetokea Ileje Mbeya? wewe ingia hapa www.ccog.org ujisomee UKWELI ulivyo.
 
Nilitegemea nitaona kanisa la kule Ileje Mbeya kumbe bado unaleta story za kimishionari kwamba Africa hakuna Mungu?

Sijui waafrika sisi tuna kazi gani hapa Duniani kama hata Mungu mwenyewe hatutambui!
Nimeona nisiendelee kubishana nae mkuu bora nawe umeliona hilo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…