#COVID19 Ukisema kuwa Tanzania haikushinda corona phase one, utakuwa muongo; huna shukrani kwa Mungu

#COVID19 Ukisema kuwa Tanzania haikushinda corona phase one, utakuwa muongo; huna shukrani kwa Mungu

ZALEMDA

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2017
Posts
1,956
Reaction score
2,225
Nimeona watu wakilaumu wakituna na wengine kudhihaki kwamba serikali haijawa serious huhusu Corona. Sisi tunaojua maana ya outbreak tunajua kwamba kwanzia mwezi wa 7 mpaka 12 hakuwa na Visa vya Corona. Wengine sisi ni watoa huduma za afya ni mashahidi kabisa kwamba Corona iliisha.

Mungu wetu mwenye huruma alituponya si kwa matendo yetu mema. Kosa letu hatukuendelea kumuomba Mungu atuponye na Corona phase 2.

Ikumbukwe kuwa kuna corona phase 1, phase 2 na phase 3. Hivyo hatuna budi kuendelea kumuomba Mungu atuponye phase 2 pia atulinde na phase 3 na tukiendelea kuchukua tahadhari pindi milipuko ikitokea.

Kumtukana Rais au kumlaumu hakusaidi kitu bala ni kuzoa dhambi bila sababu.Mkuu wa dini unapomdhihaki kiongozi wa nchi Mungu hawezi kuwa upande wako hata siku moja tena ukichukulia kuwa Rais wetu aliegemea upande wa Mungu.

Sasa sioni sababu ya kumlaumu Rais. Padri mzima unaposema eti Mungu siyo hirizi ,huo ni uchizi. Unataka kusema kuwa pale madhabahuni unasimama ukiwa umevaa hirizi .
 
Huu ujinga wenu sijui mtaendelea nao mpaka lini, Mungu amewapa akili hamtaki kuzitumia mmezubaa tu kumuachia Mungu kila kitu, muombeni Mungu basi atuondolee na huu umasikini uliotuzunguka zaidi ya miaka hamsini kwasababu ya uzito wa vichwa vyenu.
 
Hakuna popote tulipowahi kuishinda corona, sio kwa maombi wala tiba ama kumtegemea Mungu. Huyo rais mwenyewe sio mcha Mungu bali ni muigizaji akienda kanisani ili kuhadaa umma kuwa ni mcha Mungu. Kwa matendo yake hata hao viongozi wa dini wamemstukia ndio maana wanasema ukweli bila kuuma maneno.

Kilichotokea kwenye ile phase1 maambukizo hayakuwa makubwa kama sasa, na serikali iligoma kuendelea kutoa taarifa za ugonjwa. Lakini ukweli ni kuwa ugonjwa ulikuwepo na uliendelea kuua japo sio kwa kiwango cha sasa.

Kama huyo rais wako ni mcha Mungu na ameegemea kwa Mungu, kaitisha maombi juzi, ni wizara ya afya walikuwa wanafanya maigizo ya kutumia vitunguu saumu, sijui pilipili na nini.

Mbona ugonjwa ndio umezidi kushika kasi?Awamu ya kwanza serikali ilifanikiwa kulisha watu maneno ili kukwepa uwajibikaji kwa kununua vifaa tiba. Hakukuwa na cha Mungu wala kuishinda corona zaidi ya propaganda za kihuni.
 
Huyo Padre Kitima inaonekana hamwamini Mungu labda anamwamini shetani. Hata matendo yake ni ya kishetani sana tu!
Usijifanye unajua dini sana kuliki wenye dini yao.

kumwamini Mungu ni kitu kingine na matendo ni kitu kingine.

Imani bila matendo ni imani mfu.
 
Mtoa mada nilitegemea utaitoa zaidi kisayansi kumbe na wewe ni kada wa siasa,covid 19 ina hit kwa waves,nchi nyingine zimeshapigwa zaidi ya 2waves na sisi kwa sasa wave ya kwanza inatupiga,Pls pls shauri watanzania waepuke misongamano hasa isiyo muhimu,osha mikono kwa sabuni from running water na kausha mikono yako,epuka kupeleka mikono yako usoni,ukiona una dalili pls isolate yourself na mwisho vaa mask unapotaka kutoka,our no 1 sio mcha Mungu ni actor tu na angalia awamu yake watu wengi wamepotea kwenye mazingira ya ajabu wengi wameuliwa na hakuna tamko lolote kutoka kwake au polisi au JUDICIARY.
 
Nimeona watu wakilaumu wakituna na wengine kudhihaki kwamba serikali haijawa serious huhusu Corona. Sisi tunaojua maana ya outbreak tunajua kwamba kwanzia mwezi wa 7 mpaka 12 hakuwa na Visa vya Corona. Wengine sisi ni watoa huduma za afya ni mashahidi kabisa kwamba Corona iliisha..
Kwani unataka kusemaje ndugu?
 
Tunachotakiwa kufanya sasa si kumuomba Mungu aiondoe Corona round hii ya pili.Tumshukuru tu kuwa ulitushindia awamu ya kwanza na hii utatushindia.Tusimame kama Daudi alisema Mungu uliyenisaidia nikaua dubu na simba utanisaidia kuua hili filisti lipalestina linanaloitwa Goliathi
 
Huu ujinga wenu sijui mtaendelea nao mpaka lini, Mungu amewapa akili hamtaki kuzitumia mmezubaa tu kumuachia Mungu kila kitu, muombeni Mungu basi atuondolee na huu umasikini uliotuzunguka zaidi ya miaka hamsini kwasababu ya uzito wa vichwa vyenu.

usijifanye unajua dini sana kuliki wenye dini yao.
kumwamini Mungu ni kitu kingine na matendo ni kitu kingine.
imani bila matendo ni imani mfu.
Kwani dini inamilikiwa na mtu? Acha utopolo kijana!
 
Bahati mbaya umepungukiwa na uelewa juu ya neno la Mungu.

Mungu anatusaidia siku zote, wakati mwingine bila hata ya kumwomba, kwa sababu ya wema na upendo wake. Yeye huwanyeshea mvua na kuwapa mwanga wema na wabaya.

Mungu humshirikisha mwanadamu katika kila jambo, kuanzia uumbaji, uponyaji mpaka ukombozi. Kama hutaki kushiriki katika kazi zake, usitegemee kupokea neema za Mungu.

Anakupa mtoto ukioa na kushiriki tendo la ndoa, usipofanya hivyo, hata uombe na kufunga namna gani hutapata mtoto.

Anakupa chakula, ukifanya kazi. Usipofanya kazi hata ukiomba mpaja magoti yachakae, hutaiona hata kilo moja ya wali mezani.

Unaumwa malaria, tafuta dawa, mwombe Mungu. Atakuponya kwa kuwa umeshiriki katika uponyaji.

Unataka kumjua Mungu, soma biblia, nenda vyuoni ukafundishwe, nenda kanisani ukahubiriwe, mwombe Mungu akufunulie ufahamu ili uelewe unachokisoma na kukitafsiri kwa usahihi. Na kote huko utamkuta mwanadamu mwenzako anayeshiriki kazi za Mungu.

Corona phase one, kwa jitihada za kufuata maelekezo ya kitaalam, na Mungu akazibariki jitihada zile, zikaleta matokeo mazuri. Baada ya pale tukaingiwa na ujinga, tukaacha kutimiza wajibu, tukabweteka, na kutaka Mungu aendelee kutenda miujiza kwa watu wasiotimiza wajibu wao.

Mungu hutenda miujiza kila siku kwa kuwapa wanadamu karama mbalimbali, ili mwanadamu ashirrliki katika kazi za Mungu.

Toka mwanzo, Mungu alipotaka kuwakomboa wana wa Israel, kwa kupitia Musa, aliwaambia wafanye nini ili waoate kukombolewa. Walifanya kazi, waliondoka usiku, walitembea jangwani wakipitia mateso mbalimbali, na kwa kupitia jitihada hizo waliouona mkono wa Mungu.

Kukaa na kuomba bila ya kufanya kitu, bila ya kutimiza wajibu wetu, bila ya kuzitumia karama za Mungu anazozitoa kupitia wanadamu wenzetu, ni ibada za kipagani.

Msipotoshe neno la Mungu. Yatafsirini maandiko kiusahihi kwa msaada wake Mungu mwenyewe. Msiwe wajinga, mkiwa wajinga mtazikosa furaha za Duniani na mbingu hamtairithi maana Mungu hana mbingu ya wajinga. Ujinga na upumbavu siyo sehemu ya utakatifu. Mungu hujivunia watu werevu, watu wenye akili, watu wenye kuvitumia vipawa akivyowapa kwa usahihi. Neno lake linasema, yatafuteni maarifa.
 
Mleta mada hapo ndio mwisho wako wa kufikiri?

1. Mungu anapenda kila mtu awajibike kwa kutumia akili alizomjaalia na sii vinginevyo!

2. Huwezi kukaa na kutochukua hatua ie kufuata kanuni za afya wanazoshauri wataalamu eti ubaki ukisali kwa kuamini hutapata corona, never ever! utaipata na itakuua tu.

3. Hata ndege wa angani wanalishwa na Mungu lakini hawawekei chakula mdomoni bali hutoka kwenda kutafuta.

4. 'Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa', vueni makoti ya upumbavu mliyovaa labda mtakuwa na akili japo kidogo!
 
Nimeona watu wakilaumu wakituna na wengine kudhihaki kwamba serikali haijawa serious huhusu Corona. Sisi tunaojua maana ya outbreak tunajua..
Kwa ushahidi upi wa kitakwimu zilizo wazi?Bado umeng'ang'ania akili za kijima tu! Mbadilike!
 
Hakuna popote tulipowahi kuishinda corona, sio kwa maombi wala tiba ama kumtegemea Mungu. Huyo rais mwenyewe sio mcha Mungu bali ni muigizaji akienda kanisani ili kuhadaa umma kuwa ni mcha Mungu. Kwa matendo yake hata hao viongozi wa dini wamemstukia ndio maana wanasema ukweli bila kuuma maneno.

Kilichotokea kwenye ile phase1 maambukizo hayakuwa makubwa kama sasa, na serikali iligoma kuendelea kutoa taarifa za ugonjwa. Lakini ukweli ni kuwa ugonjwa ulikuwepo na uliendelea kuua japo sio kwa kiwango cha sasa. Kama huyo rais wako ni mcha Mungu na ameegemea kwa Mungu, kaitisha maombi juzi, ni wizara ya afya walikuwa wanafanya maigizo ya kutumia vitunguu saumu, sijui pilipili na nini. Mbona ugonjwa ndio umezidi kushika kasi?Awamu ya kwanza serikali ilifanikiwa kulisha watu maneno ili kukwepa uwajibikaji kwa kununua vifaa tiba. Hakukuwa na cha Mungu wala kuishinda corona zaidi ya propaganda za kihuni.
wewe ni nani mpaka una uweo wa kujua mcha mungu na mwenye imani ni yupi!!!

Mungu haangaliii unatenda dhambi kiasi gani ili akusaidie unaposali.anaangalia imani yako.
 
UKITAKA UZI WAKO UISHI HUMU SHARTI UONGEE KILA KITU NEGATIVE KUHUSU JUHUDI ZA SERIKALI HASA WAKATI HUU WA JANGA LA KORONA

HII JAMIIFORUMS IMEKUWA BIASED SANA
 
wewe ni nani mpaka una uweo wa kujua mcha mungu na mwenye imani ni yupi!!!

Mungu haangaliii unatenda dhambi kiasi gani ili akusaidie unaposali.anaangalia imani yako.

Hakuna mtu anayenajisi uchaguzi mwenye imani fullstop.
 
Back
Top Bottom