MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 14,588
- 32,361
Mimi sipingi uwepo wa VICCOBA kwasababu kwa mtu ambaye hana mtaji anaweza kujiunga na kusevu kidogo kidogo na baada ya mwaka akapata mtaji wakati wa kuvunja kiccoba. Ni njia nzuri ya kufikia malengo yako. Ila leo nitashauri watu ambao wanateseka na maisha kisa VICCOBA.
Mtu ukishaanzisha Biashara unapaswa uwekeze nguvu, pesa na akil yako yote kwenye kuikuza. Ile faida kidogo utakayoanza kuipata unatakiwa uirudishe kwenye biashara kuongezea mtaji. Biashara hadi uanze kuifaidi ina hatua nyingi ila kwa pale mwanzoni pambana sana mtaji ukue.
Itachukua muda ila ndo uhalisia. Ninapinga sana mtu ana biashara ndogo lakini hela hiyohiyo badala ya kuizungusha ikue utakuta ndo kila wiki au mwezi anaenda kupeleka kiasi kuhifadhi kwenye VICCOBA. Huo ni UPUMBAVU.
Unatunza hela ili nini wakati biashara bado changa? Wafanyabiashara wote makini hutumia benki kukopa na kulipa & kulipwa. Hakuna mfanyabiashara makini ataanza kuweka hela benki zikae tu akisubiri labda riba ya 10% kwa mwaka wakati akiweka juhudi anaweza zalisha hata 300% ya hiyo hela kwa muda huo.
Nimeandika huu uzi baada ya siku za karibuni kusumbuliwa na kina dada wengi kuhusu kuwasaidia pesa za VICCOBA. Mimi ni mtenda dhambi mstaafu kwahiyo hata kamà hawa kina dada wako tayari wanipe tamu siwezi kubaliana nao. Wafuate huu ushauri wangu. Wengi wao huishia kukopa kwingine na kujikuta kwenye mabalaa zaidi.