Ukishainuka kimaisha basi usiiname na ukiinama basi usikae kabisaa!

Ukishainuka kimaisha basi usiiname na ukiinama basi usikae kabisaa!

mathsjery

JF-Expert Member
Joined
Sep 26, 2015
Posts
2,249
Reaction score
1,813
Huwezi ishi maisha mazuri siku zote kama hauna mipango mizuri, katika kila unachofanya.

Kama umebahatika kufika mbali kimaisha yaani sio choka mbaya au fukara basi hakikisha hauwi fukara tena wala choka mbaya(yaani ikitokea umekuwa fukara na hauna roho ngumu unaweza kufa kifo kibaya kwa sababu ya wanaokuzunguka).

Hakikisha unaendelea kuwa kama ulivyo mpaka kifo kikutenge na mali zako.

Kama vipi andaa watu makini katika familia/jamaa au jamii yako watakaoendeleza juhudi zako wakati unalamba udongo na kunyonywa na funza; yaani namaanisha hivi, wewe ni nafasi ya wengine kwa usife na mali zako.

Hii itakuwa poa kwa walimwengu kwakuwa umeshaandika historia yako.

Najua haiwezi kuwa na maana kwa wachache wanaoamini juu ya hukumu siku za mwisho kama inavyoelezwa, kwa Uislamu, Ukristo n.k.

Lakini itakuwa ni ujinga kama hautajishughulisha na kupata maisha bora kwa kisingizio cha hukumu. Kumbuka hakuna kitabu cha dini kinachosema utahukumiwa kwenda jehanum kwa sababu ya utajiri na utahukumiwa kwenda mbinguni sijui peponi kwa sababu ya umasikini noooooo Ila uelezwa kuwa dhambi ndio sababu, si ndio wanatheolojia?

So, the main point ni kutengeneza historia nzuri yenye mfano wa kuigwa. Ukishainuka mwenyewe usikubali ukalishwe chini labda ukae mwenyewe na ukijaribu kufanya hivyo, basi jikaze.
 
Kisha nikafikiri na kuona sio wenye akili sana wapatao mali, wala si wajinga tu wafao kwa njaa... yote haya ni ubatili mtupu chini ya jua.

Hapo kwenye 'kunyonywa' na funza ndo kitu cha muhimu, mizoga ni mbolea iliyotukuka... kujengea makaburi na matumizi mabaya ya virutubisho.
 
Ni rahisi sana kufanikiwa, ila inahitaji umakini wa hali ya juu kuendelea kubakia kwenye hayo mafanikio...




Cc: mahondaw
 
Back
Top Bottom