sifi leo
JF-Expert Member
- Mar 30, 2012
- 5,182
- 8,948
Kwa kweli nalilaani tetemeko la ardhi lililotokea Bukoba na kusababisha vifo vya baba, mama, bibi, anko, shangazi na wadogo zangu. Pia ninalaani vikali wale waliotumia rambi rambi zilizochangwa na ndugu na jamaa wema kwa wahanga wa tetemeko kutumika kuboresha magereza mkoani Kagera.
"Hivi nyinyi Wahaya kila kitu nyinyi tu, Ukimwi nyinyi, mto ngono nyinyi, katerero nyinyi, na sasa tetemeko nalo nyinyi tu."
Maneno haya niliyasikia kwa masikio yangu kutoka mdomoni mwa kiongozi mkuu wa nchi aliyekwenda mkoani Kagera kuwafariji wahanga wa tetemeko. Aliongeza kwa kusema:
"Sasa nimeelekeza michango ya rambi rambi ikaboreshe yale magereza yawe safi, yaboreshe na ile shule niliyosoma mimi. Sina hela ya mchezo-mchezo ya kugawa kwenu, tetemeko halikuletwa na CCM." Mwisho wa kunukuu.
"Sasa naboresha gereza ili mliobolewa nyumba zenu na tetemeko mkienda kuibiana, mkamatwe na mfungwe pazuri."
Hapo nilisikia wazee wa Kichaga wakizungumza kwa kilugha huku wakiondoka uwanja wa Kaitaba kumsusia mkutano wake, wakisema:
"Tugende heki nekilalu, tikigira magezi, nekinywa njai."
"Hata msipo nisikiliza mkaondoka mkutanoni, maneno yangu mtakutana nayo kwenye TV saa mbili kwenye taarifa ya habari."
Msemaji waweza usinielewe. Hivi nauliza, Wasukuma wakoje?
Wakati tunastaajabu ya Hayati Magufuli kujenga kanisa kwenye eneo lake na kulizungushia ukuta mrefu huku akijiamulia kanisa liitwe Mtakatifu Josep wa Kishoiya na kulikabidhi kwa Kanisa Katoliki — lakini kanisa hilo likalikataa jengo hilo — jana nimeshangaa jengo kubwa la polisi ambalo, kwa mujibu wa wananchi, lilijengwa na mbunge wao yule anayejiita mbunge asiye na elimu, yaani Msukuma, na kulikabidhi kwa jeshi la polisi huku likikataliwa na wananchi.
Kwanza, hivi wananchi wanachagua viongozi ili wawajengee sehemu za kuwafungia? Kwa nini wananchi wamekataa kituo cha polisi?
Kwa mujibu wa mwanakijiji mmoja, anasema kijiji kilitenga eneo la kujenga kituo, lakini mbunge huyo akahamisha wazo la kujenga kituo katika eneo lililopendekezwa na wananchi na kwenda kujenga kituo karibu na nyumbani kwake ili kumrahisishia ulinzi pale anapokuwa kwake.
"Yaani hawa Wasukuma hatuwaelewi. Tunawachagua sisi alafu wanatuogopa sisi. Huyu King Msukuma alijenga kituo cha polisi hapa karibu na kwake badala ya pale tulipopataka sisi wananchi na kutenga eneo. Hata Hayati Magufuli naye aliwahi kujenga kanisa nyumbani kwake tena Katoliki. Hivi wewe uliwahi kuona kanisa Katoliki nyumbani kwa mtu? Hata Hayati pia alijenga bonge la kituo cha polisi pale kwake Chato, kina kamera mpaka ndani ya nyumba yake. Sasa najiuliza, hawa watu wanatuogopa sisi tuliowachagua?"
Ebu jiulize ndugu yangu: "Majigambo ya mbunge King Msukuma kwenye vyombo vya habari, unaweza kuamini anaongoza jimbo lisilo na hata hatua moja ya barabara ya lami? Basi lami ni gharama, tufanye bomba moja la maji kutoka Ziwa Victoria mpaka hapa kituo cha polisi alichojijengea yeye, mkewe na watoro wake, maana sisi tumekikataa na polisi tumewafukuza."
"Sifi leo tunakuonaga mnamhoji Mbunge Msukuma huko bungeni. Hivi hata ongea yake, mavazi yake, na maneno yake mengi, unaweza kuamini hapa Nkome, Nzera na kwingineko ndio jimboni kwa King Msukuma?"