Naomba nianze kwa kutoa credit kwa member wa humu jamii forum aliyeandika hiyo title. Kwa kweli imenigusa sana mpaka nikashawishika kuitengenezea mada tofauti.
Ebu jiulize ni wangapi wameweza kuexcell na kufanikiwa kimaisha na kimaendeleo kwa haraka zaidi ya wanasiasa na Machawa kwa miaka 5 iliyopita. Ebu angalia ma-deals na ma-promotion mengi yako kwa akina nani ebu angalia wanaonunua magari ya maana na kujenga majumba za ghalama zaidi ya wanasiasa na Machawa ni akina nani zaidi(angalizo-haimaanishi kufanya hivyo ni kutusua bali ni viashiria vya kufanikiwa). Je wasomi wangapi wametusua kwa haraka kwa kipindi kifupi hiki tulichopitia kama hawa majamaa...
Kuna kipindi nafikiri cha awamu ya pili , wafanyabiashara walitusua sana, ni kipindi cha Mh Mwinyi, wasomi wakabaki nyuma sanaaaaa; wengi tukaona hakuna haja ya kusoma, kuna vjana walihishia njiani wakaenda kwenye biashara, wengine walitusua , wengine ndio hivyo tena. Ikafuata awamu ya tatu, huyu bwana akaleta heshima ya wasomi, awamu ya nne, awamu ya mzee wa Kisoga, mzee wa Chalinze, mzee wa mishemishe akaendeleza mtindo uleule, tuaziita enzi za mishemishe. Ni kipindi cha Magufuli zaidi na taratibu wasomi wakaanza kutambulika tena kidogo kidogo na elimu ikaanza kupewa heshima kwa mbali.
Ila kwa awamu tuliyopo sasa naona suala la Machawa limetamalaki. Yaani nakuambia ndio habari ya mjini. Kibaya zaidi Impression mbaya ninayoiona ni vijana wengi kuingia kwenye uchawa, na nakuhakikishia hata humu ndani wameshaanza kujipendekeza. Unakuta kijana hoja inaeleweka ni dhuluma, ni wizi wa waziwazi, ni udhalilishaji lakini kijana msomi, kijana mwenye akili timmu, kwa sababu ishu zimefanywa na wapendwa wao wa kisiasa huku wakitegemea kupromotiwa, wako tayari kujitoa akili na kutetea uhozo wa ajabu unaoendelea, tena kwa point za kujidhalilisha.
Kwa wewe msomaji lazima ujue ili kuwa chawa maridadi lazima uwe na uwezo wakujidhalilisha; ni sawa na ili uweze kuwa mchawi mashuhuri lazima uweze kutoa kafara, kumuhasi Mungu, Ebu jikumbushe ni machawa wangapi wameweza kufikia hapa walipo , ukuu wa mikoa, ujumbe wa almshauri kuu, uwaziri, baada ya kutesa, kudhalilisha, kuua wengine, kulamba miguu na makombo ya wengine. n.k
Hofu yangu, amini nawaambia dalili za nchi kuanza kuhangamia ni pamoja na nguvu kazi, nguvu kazi ya vijana kuelekea kwenye uchawa. narudia ili uwe chawa lazima ujitoe akili, uwe tayari kusacrifice wengine wooote kwa personal benefits/gain. Sasa hiyo ndiyo Tanzania ya citirical thinkers itakavyopotea.