Ukishaweka mfumo wa umeme kwenye nyumba yako tafuta mtu akulindie

Equation x

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2017
Posts
33,679
Reaction score
49,841
Nimekuwa mhanga kwenye hayo mazingira, baada ya kufanya 'wiring' na umeme kuungwa kwenye jengo, ili ujenzi wa kumalizia (finishing) uende vizuri; wakatokea wahuni wakakata nondo za dirisha na kuingia ndani na kuanza kufumua nyaya zote, pamoja na vifaa vyote vya umeme vilivyokuwepo.

Ile vijana wangu wanaenda kukagua, ndio wakakutana na huo uaribifu. Kwa ujumla wamenipa hasara, lakini ndio hivyo inabidi kukubali matokeo.

Kwa ushauri tu, kama umefikia hatua hiyo, tafuta mtu akulindie, vinginevyo wahuni wanaweza kukutembelea wakakuachia mabomba tu.​
 
Huu michezo Moshi umeshika hatamu na hii inachangiwa sana na kuwa kwa Sasa waya zinapitishwa kwenye mabomba TU hivyo ni rahisi kuchomoa.....
Zamani waya inatembea kufata mbao za ceiling board na clip za kutosha...
 
Hii imetokea Arusha wiki mbili zilizopita
 
Nimekuwa mhanga kwenye hayo mazingira, baada ya kufanya 'wiring' na umeme kuungwa kwenye jengo, ili ujenzi wa kumalizia (finishing) uende vizuri; wakatokea wahuni wakakata nondo za dirisha na kuingia ndani na kuanza kufumua nyaya zote, pamoja na vifaa vyote vya umeme vilivyokuwepo.

Ile vijana wangu wanaenda kukagua, ndio wakakutana na huo uaribifu. Kwa ujumla wamenipa hasara, lakini ndio hivyo inabidi kukubali matokeo.

Kwa ushauri tu, kama umefikia hatua hiyo, tafuta mtu akulindie, vinginevyo wahuni wanaweza kukutembelea wakakuachia mabomba tu.​
Uwekaji wa umeme una phase mbili, phase ya kwanza ni kuchimbia bomba kwenye kuta na phase ya pili ndio Wiring

Phase ya kwanza unaweza ukaifanya kabla hujahamia, lakini phase ya pili inatakiwa uweke baada ya kuhamia (Mlinzi unaweza ukamuweka lakini nae pia ni binadamu, anaweza akapuliziwa dawa ya usingizi na wezi wakaiba kama kawaida)
 
Ni muhimu sana kuzingatia
 
mkuu wa kazi pole sana. inaumiza wezi wanarudisha nyuma sana. namna hii ukimfanyia mtu ukatili aje kulalamika baadaye
Wanarudisha nyuma sana, muhimu kujihami kabla kama inawezekana.
 
Back
Top Bottom