Ukishiba usisahau wenye njaa

Ukishiba usisahau wenye njaa

Real64

Member
Joined
Feb 17, 2014
Posts
28
Reaction score
32
Ukiwa kwenye mfumo au nje ya mfumo na una connection, huwezi kuona umuhimu wa baadhi ya sheria kufanyiwa marekebisho. Ukiwa kwenye mfumo ni rahisi kuwafahamu baadhi ya watendaji walio katika sekta mbalimbali vivo hivyo ukiwa nje ya mfumo na una connection ndani ya mfumo ukiwa na shida yoyote utakuwa unateleza tu. Maana hiyo huwezi kuona umuhimu wowote wa baadhi ya sheria kufanyiwa marekebisho.

Tujiulize ulize swali, hivi tumeshafikiria madhila wanayopata watu walio nje ya mfumo na hawana connection? Fikiria leo hii ukitaka kupitishiwa leseni yako au kubadili madaraja ya leseni yako ni lazima uende mkoani?

Ni usumbufu kiasi gani watu wanapata?Hakuna uwezekano wa haya yote kufanyika wakiwa huko huko wilayani kwao?Kuna haja kwa watunga sheria kuzipitia sheria zote na kama zina mapungufu basi zifanyiwe marekebisho maana haziendani na uhalisia wa maisha ya sasa.
 
Back
Top Bottom