Ukishikamana na Mchina atakunyonya hadi Ukome, ukishikamana na Mmarekani atakuhujumu hadi Ujute je, yupi ni sahihi Kwetu Kimaendeleo?

MINOCYCLINE

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2015
Posts
8,018
Reaction score
16,802
Kazi yangu kubwa leo katika huu Uzi ni kusoma tu Maoni ( Comments ) za JamiiForums Great Thinkers (Werevu ) ili nami nijue na nijifunze mengi kisha nije kuwa kama nyie.

Karibuni nikitumai na walioko Washington sasa ikiwa ni saa 6 ikienda saa 7 za Usiku kama bado hawajalala watapata nafasi ya Kusoma Maoni yenu ili wajue Rafiki Bora wa Kutufaa Tanzania kati ya Mmarekani Mhujumu na Mchina Mnyonyaji ni yupi.
 
Mchina sio mnyonyaji tu ,bali pia ni mwizi, bora ufanye kazi na mmarekani
 
Kwahiyo unapenda Kuhujumiwa na Mmarekani? Sawa.
Hujuma zipo kila mahala hata nyumbani kwako kiaina unaweza ukawa unahujumiwa na mkeo, ni swala la kujipanga na ku deal nalo tu.
Mnyonyaji hana huruma kabisa na wewe na lengo lake ni uchoke upotee abaki yeye
Wachina wanaipenda sana ardhi ya Africa , ila hawataki sisi tuwemo kwenye ardhi hiyo
 
Marekani ni sahihi, nchi zote zilizoshirikiana nae zina maendeleo Japan,china, Malasyia, falme za kiarabu, South Korea,nk. Hata bongo tu ukiajiriwa na Mmarekani analipa maslai mazuri ya utu ( mshahara,posho,bima, nyumba, usafiri,nk,kuliko Mchina
 
Kwahiyo unapenda Kuhujumiwa na Mmarekani? Sawa.
Hujuma zisizoumiza kabla ya ujio wa jiwe life ya migodini ilikuwa tamu hatari.Kazi wiki sita then off wiki tatu kale bata urefresh mind urudi mpya kazini.
 
Yaani hakuna mahali natamani kufanya kazi kama US Embassy..., lila post zinazonihusu wakitoa huwa naomba bila kuchoka lakini sijawahi hata kuitwa kwenye interview. So sad ila naamini one day yes

Sent from my SM-J415F using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…