Paulsylvester
JF-Expert Member
- Oct 15, 2021
- 1,464
- 3,379
Serikali inamipango mibovu sana juu ya wakulima wa nchi hii
Ni uonevu juu ya uonevu!! Haya mambo ifike mahali tuone aibu kwa kuwanyonya kiasi hiki wakulima
Wakulima wa nchi hii, ni wao tu ndio wanaojua mateso wanayoyapitia, kwenye jua Kali na mvua za radi na Mawe, wao na shamba,
Kwenye mvua kubwa na haba, wao na shamba, wamebeba msalaba mzito huku wakiwa na matumaini ya kuendeleza familia zao, lakini wanakwamishwa na mipango mibovu ya serikali yao masikini ya Mungu!!
Kila mtu ukimuuliza, atatoa takwimu kusema, nchi yetu hutegemea kilimo kwa zaidi ya 70℅ na wananchi wengi ndio hutegemea kilimo kwa ajili ya kujikimu maisha yao, kusomesha na kuendeleza familia zao
Sera ya nchi yetu inasema, Nchi yetu ni ya wakulima na wafanya kazi!!
Serikali ituambie, kwa nini bunge letu halima MTU wa kuwasemea wakulima? Badala yake wanawekewa mawaziri ambao hata shamba hawana, hawajui kulima na hawaujui uchungu wa wakulima wanaoupitia...?
Serikali na waajiriwa wake, kila mwaka wafanya kazi wa serikali hulia kuongezewa mishahara, posho na fedha sijui za kujikimu kwenda safari za kuwatazama wanavyolima n.k
Lakini ukirudi kwa wakulima, hayupo hata mmoja anayefikiria kuweka mfumo wa angalau wa kuwapatia ruzuku wakulima hawa, Hiii wagosha
Wakitaka kuuza mazao yao wenyewe waliyoyalima wao wenyewe kwa jasho lao na kwa damu, utasikia mtu anasema, niskie mtu akipandisha bei ya vyakula! sijui niskikie mtu akifungua mipaka ya kuuza mazao nje!!! mbona tunavunana kiasi hiki?? Yaani hatuoni kwamba kuna mtu anakula jasho la mtu bila lidhaa yake?
Huu ni uonevu wa hali ya juu kwa serikali, na haiwezekani,
Inakuwaje kwenu nyinyi wafanya kazi mjiongezee mishahara na maposho yasiyo na maelezo, na muone ni halali kwenu, ila kwa wakulima kuuza kwa bei wanayoitaka iwe ni haramu.....?
Ni kwa sababu mawaziri wote wanaopewa wizara hiyo, si wakulima ndiyo maana! hawajui hata jembe linashikwaje, hawajui madhila yoote wayapatayo wakulima..?
Mambo wanayofanyiwa wakulima ni kwa sababu hawana wa kuwasemea bungeni??
Leo hii wanalia mbolea hakuna, na kama zipo, bei zake zimewashinda, lakini wanalima hivyohivyo, wakija kupata tumazao twao, mnawazuia wasiuze kwa bei waitakayo,
Je, wakulima wa nchi hii wataendelea lini?? Ni lini wataondokana na umasikini..?
Wapelekeni basi angalau mabwawa tuu ili wawe wanalima Mara kwa Mara muone kama wengi wenu hamtahamia kwenye kilimo, napo hamtaki!!! Hii wagoshaa ujue inauma eeeh!!
Mijini ndiko kwenye viwanda, na vitu Bei ya chini kwa vitu vitokanavyo na malighafi zilezile za mkulima, na ndiko huko ambako wakulima hawakai, malighafi zilezile zikirudi kwa mkulima, mama yangu, anauziwa kwa kukomolewa ili tu aendelee kuwa masikini!!
Hivi serikali mnajua kwamba, umasikini wa wakulima wa nchi hii mmewasababishia nyinyi??
Ingelikuwa ni heri sasa, Serikali ichukue hatua kuliona hili na kulifanyia kazi haraka Kabla ya wakulima hawajaamka na kusababisha sntofahamu!!
Tusitengenezee umasikini, unafanya kazi serikalini, fanya na ule kwa urefu wa kamba yako, kwa nini mkulima hamtaki ale kwa urefu wa kama yake na badala yake mnamfanya awe adui mazao yake yanapokuwa tayari kwa kuuzwa?
Mungu Ibariki Tanzania