Ukistaajabu ya Musa... Singano to TP Mazembe dau la usajili ni tshs 115 m

Haina Ela ukiifananisha na Timu gani, naomba utuwekee hapa makusanyo yote ya mlangoni, televisheni na mgao wa CAF hapa tuamini usemayo
Haina fedha kwa maana hawapati tena fedha za Mose katumbi kama walivyokuwa wakizipata awali!

Mose katumbi anaishi ufaransa hakai tena DRC yani yupo mguu ndani mguu nje kwenye kuifadhili Tupuise mazembe, timu kubwa kama Mazembe haitegemei mapato ya milangoni kama vilabu vya Bongo leo imefedheheshwa na Azam fc
 
unaweza kutaja kikosi cha TP Mazembe walioshiriki Kagame cup pale Rwanda??? au unakurupuka tu...
 
unaweza kutaja kikosi cha TP Mazembe walioshiriki Kagame cup pale Rwanda??? au unakurupuka tu...
Yani kikosi kilichecheza na Azam kimekosa wachezaji wa first 11 ya Tp mazembe sio zaidi ya watano!

Na wengi wamekwishasajiliwa kwingine, mimi mpira naujua kuliko unavyofikiria
 
Yani kikosi kilichecheza na Azam kimekosa wachezaji wa first 11 ya Tp mazembe sio zaidi ya watano!

Na wengi wamekwishasajiliwa kwingine, mimi mpira naujua kuliko unavyofikiria
acha uongo.....UNAJUA HAPA NAFIKIRIA NINI??
 
acha uongo.....UNAJUA HAPA NAFIKIRIA NINI??
Yani ukitaka kubishana na mimi kuhusu michezo hasa soccer, american football, rugby na tennis utakwama buda!

Kalaba, Muleka, Kouame, Sinkala, Zola....wote walikuwepo hawa ni wachezaji wa kikosi cha kwanza wengine walikuwa timu ya taifa na wamepewa mapumziko
 
ok... poa.
 
Hii team sio mbovu watanzania tunasahau sana yani hii ilimpiga mtu 8 caf chapions wamefugwa kimpila tu
 

Moise kasharudi Congo, Mazembe hawajashuka sema kile kikosi chako matata kimepita kwa umri, sasa hivi wanatengeneza timu upya, juzi tu wamemuuza Elia kwenda ulaya
 
Katumbi amerudi Lubumbashi
 
Moise kasharudi Congo, Mazembe hawajashuka sema kile kikosi chako matata kimepita kwa umri, sasa hivi wanatengeneza timu upya, juzi tu wamemuuza Elia kwenda ulaya
Nimesema Mose haishi Congo kama makazi yake kama alivyokuwa akifanya wakati wa Kabila kabla hajatibuana nae!

Congo anaenda kwa biashara zake tu na ikiwemo Tupuise mazembe ambayo haifadhili kwa kiasi kikubwa sasa yani ni kama hategemei return kubwa kutoka kwao tena
 
Unataka kutuaminisha kwamba Moise Katumbi amefilisika?? Au amegoma kutoa pesa kwa ajili ya udhamini? Umeandika mtizamo wako au unao uhakika kutoka chanzo cha kuaminika? Je unamfahamu Mmiliki wa TP Mazembe? Unafahamu kwamba TP Mazembe ni timu inayomilikiwa na Binadamu mmoja Mwenye migodi kama yote kule Wantashi na Investiment za kutosha kule Ubelgiji na Ufaransa?Na anaupenda mpira wa miguu kutoka moyoni?Unafahamu kwamba waziri wa michezo wa Congo ni kocha wa Makipa wa TP Mazembe?
 
Unataka kutuaminisha kwamba Moise Katumbi amefilisika??
Hajafilisika ila ana tatizo na serikali ya Congo hayuko salama kabisa hivyo uwekezaji wake mwingi anaupa nguvu nje ya nchi kuliko ilivyokuwa ndani

Au amegoma kutoa pesa kwa ajili ya udhamini?
Hatoi fedha za kununua wachezaji ghali tena

Umeandika mtizamo wako au unao uhakika kutoka chanzo cha kuaminika?
Ndivyo ilivyo

Je unamfahamu Mmiliki wa TP Mazembe?
Moise katumbi

Unafahamu kwamba TP Mazembe ni timu inayomilikiwa na Binadamu mmoja Mwenye migodi kama yote kule Wantashi na Investiment za kutosha kule Ubelgiji na Ufaransa?
Kumiliki migodi au kutokumiliki si hoja, hoja ni hatoi fedha za kununua wachezaji ghali ambao atawalipa mishahara ghali ili klabu ifanye vizuri

Na anaupenda mpira wa miguu kutoka moyoni?
Hili swali anaweza kulijibu yeye binafsi nachofahamu ni mfanyabiashara na pale anasaka pesa

Unafahamu kwamba waziri wa michezo wa Congo ni kocha wa Makipa wa TP Mazembe?
Anaitwa Robert kidiaba mbunge wa katanga na ukicha wake ulikoma pindi tu alipoteuliwa kuwa waziri wa michezo na Rais Felix Tshisekedi
 
Umejibu vizuri sana....Nimekugongea like[emoji41]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…