Ukistaajabu ya Musa utashangaa ya Firauni; aliyesingiziwa kufa aomba rambirambi zake huko Mtwara!

Ukistaajabu ya Musa utashangaa ya Firauni; aliyesingiziwa kufa aomba rambirambi zake huko Mtwara!

WhoWeBe

JF-Expert Member
Joined
Dec 18, 2022
Posts
2,299
Reaction score
4,282
Taharuki yatanda kwa wananchi wa kijiji na kata ya Nanganga mkoani Mtwara, baada ya kupata taarifa ya kifo cha Simon Mchekura maarufu ‘Samora’ ambaye mwili wake ulidaiwa kuokotwa na Jeshi la Polisi katika kijiji cha Nyengedi, mkoani Lindi, na kuhifadhi kwenye Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Lindi Sokoine wakisubiriwa ndugu zake.

Akizungumza na ITV ndugu wa marehemu aliyedaiwa kufariki dunia Bw. Wakati Mchekura, amesema walipata taarifa siku ya tarehe sita na tarehe Saba mwezi huu wa sita mwaka 2023, wakati wakiendelea harakati za mazishi baada ya kwenda kuuchukua mwili Hospitali ya Sokoine, wakapata taarifa kwa njia ya simu kuwa huyo wanayetaka kumzika, sio ndugu yao ila ndugu yao ameonekana kwenye maeneo ya vijiji vya Rondo, akiwa anakunywa pombe ndipo walipochukua pikipiki na kumfata na kumleta kijijini hapo.

Ukistaajabu ya Mussa utayaona ya filauni, yule aliyesadikiwa amefariki dunia Bw. Saimon Mchekura, baada ya kuletwa pale nyumbani na kukuta watu wengi, na alipouliza na kupatiwa jibu kuwa watu hao wamekusanyika hapo kwa ajili yake ya mazishi ya mtu waliomfananisha aliomba apewe rambirambi zilizokusanywa kwenye msiba huo😂😂😂😂😂👆🏼👆🏼👆🏼👆🏼👆🏼👆🏼
 
Njaa mbaya sana jamaa ameona isiwe shida nipeni changu mapeeema [emoji23]
 
Fursa kaona ni rambirambi...

[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Back
Top Bottom