Ukitaka biashara yako ifilisike mapema ajiri marafiki kwenye biashara

Money Stunna

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2011
Posts
13,053
Reaction score
6,304
Nasema hivi kutokana na uzoefu wangu pia yalinikuta,nashauri ukitaka kuajiri mtu ajiri mtu ambaye si rafiki yako kwenye biashara zako ndio ata kuheshimu na kujali biashara zako,hapo mwanzo mimi niliweka marafiki kutokana na kuwa hawana kazi za kufanya pia kama kuwasaidia lakini nilihishia kugombana nao,pia kuwatimua kazi na mpaka sasa hatuongei kutokana na upuuzi waliokuwa wanaufanya na walisahau nilipowatoa wakajua kampuni ni yao.

Ajiri mtu ambaye si rafik yako atakuheshimu sababu atajua akichemsha utamtimua haraka tofauti na marafiki ambao wengi ni wanafiki tu watajua uwezi kuwaqfanya kitu sababu ya urafiki wenu.

Huo ndio ushauri wangu si lazima ukubari ila marafiki ni wakuwa nao macho sana wengi si watu wazuri
 
Wanaweza wakawa watu wazuri tu ila sio sahihi kwani huwezi kuwaonya na wao wanachukulia mazoea hakuna hofu wala heshima. Hiyo inafanya hata wafanyakazi wengine kushuka morali na biashara kuharibika
 
Bora umuweke mkeo shanging shanging lile lol
 
naunga mkono hoja 100% . yaani marafiki na ndugu mara chache sana kuheshimu na kuinyenyekea biashara yako kama ipasavyo, kadhalika na pesa zako! mwisho wa siku pesa wanakula na biashara wanaiua. sisemi ndugu au marafiki wote, bora hata ndugu wadogo. nimegundua ndio maana wachaga wengi huweka wake zao au watoto katika biashara zao, wameliona hili. big up chaggaz!
 

Tena ni bora ndugu wa kuzaliwa lakin awa wengine sijui binamu etc hawana adabu kabisa na mali ya mtu
 
Hii ni 100% proved valid! wanamajungu na always they deliberately exert as much as they can to knock you down n start loughing at you!
 
Kuna ukweli mkubwa sana katika hili aiseee Biashara nyingi zinakufa kutokana na kukosa nidhamu ya pesa na ya kibiashara, chanzo ni ndugu na marafiki wa karibu
 
na usipowapa shavu majungu kama kawa jamaa ana roho mbaya sana huyu ubinadamu kazi!
 

Mi nafkiri ndugu kidogo ndio vigumu kum manage na kumbana endapo akiharibu biashara yako. Ila kama ni rafiki yangu ukizingua mi nakupoteza tu, nakufanyia na hela yangu utarudisha. Istoshe mi sitaki mazoea sana na watu unless its a person from the inner circle ( Am cautious with such people though ). Tokea niponee chupu chupu kuingizwa mkenge na mwanamke wangu wa zamani mamilioni ya hela, hyo experience imenifanya niwe na roho ngumu sanaaa and all i trust is JESUS. All in all ur advice is Great !!
Thanks in advance !!
 
How true.

Nilikuwa na mshkaji wa miaka mingi ambae alikuwa na experience sana na shughuli zetu, lakini namwambia please please naomba ufanye ninavyosema kwa sababu mi ndio jina langu liko kwenye ma leseni huko, kikiharibika kitu hapa naweza hata kufungwa au tukipoteza contract mimi ndio nitabaki na mavifaa na ma payroll na ma rent yameni dodea hapa, nataka niwe fully responsible with how things run here, please nisikilize, jamaa haelewi! Nikam fire! Hakuamini. Sasa ni maadui, hatuongei, hatupishani njiani, hatusalimiani. So sad.

But then the question is mshkaji anakufata hana ajira, mwanao kabisa miaka michache mlikuwa mnakaa pamoja mnashauriana nini cha kufanya, sasa wewe umepiga hatua kidogo, unamtoleaje nje kazi?
 

Cha muhimu lazima uchague unataka biashara yako ifanikiwe au unataka kuwafuraisha marafik
 
Mbona wahindi wanaweza? Ndugu wa familia ndo mara nyingi naona wanaendesha biashara!

Nadhani cha msingi hapa ni kuwa na marafiki serious ambao nao wame risk capital yao kwenye biashara husika. Na kwamba wakicheza nao wanapoteza pesa yao. Afu angalia msiwe marafiki wengi sana kwani huwa inaleta shida. At least muwe watatu, na kila mtu aweke capital ya kutosha.
 

Wahindi toka wakiwa watoto akitoka shule basi lazima ataenda dukani na kwa jinsi anavyokuwa anakuwa anamsaidia mzazi wake kwenye biashara hivo wana discipline za pesa.

Kuhusu ilo lingine ulilosema uko sahihi
 
Kuna rafiki yangu nlimtumia 1.5mil il aninunulie vifaa vya stationery Dar amekula hadi hv ss hapatikani yaan watu wanatumia urafiki kukutia hasara wanajua hutawafanya kitu!!!
 
Kuna rafiki yangu nlimtumia 1.5mil il aninunulie vifaa vya stationery Dar amekula hadi hv ss hapatikani yaan watu wanatumia urafiki kukutia hasara wanajua hutawafanya kitu!!!

pole sana
 
Ndugu, Marafiki, Tumbo moja wako, Mtu wa karibu ni kero tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…