Tomaa Mireni
JF-Expert Member
- Sep 8, 2015
- 2,395
- 2,391
Heshima kwenu wasomaji na wapiga kura.
Leo nataka niwape vijana fursa ambayo kwa miaka imedharaulika.
Biashara ya maduka ya vyakula inaweza kumtoa mtu yeyote yule lakini inategemea na eneo na moyo wako wa kuifanya.
UMUHIMU WA KUFANYA UTAFITI KWANZA
Kuna maeneo yanayotifautina sana mahitaji,duka la Mbezi Beach ni tofauti na la Mbagala. Zingatia hiyo unapotafuta mazingira usije ukaweka bidhaa zikaoezea dukani.
TAHADHARI.
Usiifanye biashara yoyote kwa sababu unasikia ina hela au imemtoa fulani. Fanya biashara utakayoipenda na kuithamini na kuifanya kwa bidii na moyo wote,sio kwa sababu una shida.
Biashara hii huwa inabadana sana muda,yani ukiamua kuifanya hakikisha muda wako 90% upo dukani,na 10% kulala tu bila hivyo utakuwa unacheza.
ANZA HIVI UNAPOKUWA NA MTAJI WAKO
1. Fanya utafiti wa eneo la kuweka duka lako, kwanini? Sababu unaweza kufungua sehemu ambayo tayari kuna watu wakubwa(matajiri waliokuzidi kwa hiyo ukaambulia kupiga mihayo tu na mwishowe ukafunga.
2. Tambua uhitaji wa eneo hilo,yani unaweza kutumia hata wiki ukitafiti eneo hilo lina maduka mangapi? Yana ukubwa gani? Je yanatosheleza mahitaji kwa wakaazi au kuna uhitaji wa duka lingine! Kama kuna uhitaji linganisha nguvu yako na uliyoikuta.
3.Tafuta fremu yako eneo husika na weka mali dukani baada ya kujiridhisha.
4. Vumilia kupata faida hata mwezi mmoja ili uvute wateja kwa bei nafuu na ofa mbalimbali. Ongea vizuri na wateja kama kwamba unataka kuwasaidia lakini kuwa makini sana na mitego yao. Epuka kabisa kumtongoza mteja hutafika mbali.
Ukishazoeleweka kuwa wa bei chee hata ukija kupandisha hawatajua sababu tayari wamekuzoea.
5. Mwisho cheza na majirani zako vizuri,kuwa na ujirani mwema,ila cheza na akili yao,angalia kasoro zao kwa mteja ww zirekebishe,angali bidhaa gani hawana na inatakiwa anza kuiweka wewe wao wakufuate.
TAMBUA HAKUNA BIASHARA ISIYO NA MIKOPO.
Kopesha wateja kwa kila mmoja na kiwango chake(angalia matumizi ya mteja kila wakati,[kuwa makini hapa]sio wote watalipa) huwezi kukwepa mikopo sababu na wewe lazma ukope huko unakonunua pia,siku hazifanani.
Thamini kila shilingi usichukulie powa 50 ukaona sarafu ndogo haikupunguzii kitu,ogopa sana mteja anaerahisisha maisha kwa kuidharau hiyo pesa hafai hata kukopeshwa sababu anataka ufunge duka akuhame.
HITIMISHO
Msingi wako utategemea na eneo ulilopata kufanya biashara. Kuna sehemu ukiwa na 1m unatoka kabisa bila garama za marekebisho ya frem na kodi ya pango, sehemu nyingine hiyo ni robo tu na haitoshi kabisa.
Karibu na asanteni kwa usomaji, msisahau kunipa kura yenu tafadhali huenda nikaboost kiduka changu kipya ambacho nimeanza na 500k tu😁.

Upvote
20