Ukitaka kuishi maisha mazuri na yenye furaha zingatia haya

Ukitaka kuishi maisha mazuri na yenye furaha zingatia haya

The redemeer

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2025
Posts
1,497
Reaction score
2,681
👇🏻

1.> Jikubali kuwa unaweza, na unaweza kuwa yeyote muda na wakati wowote.

2.> Epuka kuishi maisha ya kuigiza, ishi maisha yako halisi.

3.>Usiishi Maisha ya kushindana, yatakupelekea kuwa mtumwa wa kudumu.

4.> Asilimia 90, ya Maisha ya watu mitandaoni sio halisi.
Hivyo Yasikufanye ukajiona si' lolote. {Shika hilo.}

5.> Jifunze kuto ng'ang'ania vitu, Jifunze kuachilia baadhi ya mambo kwenye maisha yako.

6.> jifunze kutoshirikisha kila mtu shida yako.

7.> Jizoeze tabia ya kusamehe na kusahau.

8.> Epuka tabia za majivuno hata kama ulichonacho Wenzio hawana.

9.> Sio kila mtu, anafaa kujua vyanzo vyako vya mapato, Mafanikio ni kama nguo ya ndani haipaswi kuonwa na kila mtu.

10.> Using'ang'anie kinachokuumiza, tafuta njia nzuri ya kukiepuka, ikiwa kipo nje ya uwezo wako.

11.> Mwisho; Hakuna rafiki Mzuri na mwema kwako kama wewe mwenyewe.

Huhitaji kuwaamini wengine kama vile unavyohitaji kujiamini ili kufanya maamuzi sahihi.

#Topaz ✍🏿..
 
Ndani ya gereza Moja pale Brooklyn Kuna maandishi yanasema
"No one is your enemy but everyone is your teacher trying to teach you the principles of life"
Kwenye Kila changamoto usitengeneze adui we jifunze kutokana na rafiki mbaya
 
No 1 na No 2 zina contradiction...

Yani naweza kuwa kama yeyote lets say kama Ronaldo alafu no 2 inasema niishi maisha yangu

Kvp nataka kuwa kama ronaldo alafu niishi maisha yangu? Lazma niishi kama Ronaldo ili niweze kuwa kama Ronaldo

N.B FAKE IT UNTIL YOU MAKE IT Brothers
 
Back
Top Bottom