mkaamweusi
JF-Expert Member
- Feb 19, 2013
- 618
- 824
Ndio,njaa ni tatizo namba moja ambalo inatakiwa ulishinde kabla ya kuwaza maendeleo,yaani kwa wale wanao anza maisha ni vema kwanza kabla hujaana kuwaza maendeleo hakikisha unaunda mechanism au mfumo flani ambao utakuwezesha kugharamia kula na lala yako,baada ya hapo anza kujitanua,kufikiria kutengeneza mifumo ya kugharamia safari zako za nje,mapumziko,ada za watoto wako na wengine,wazazi wa pande zote mbili.
Ukishindwa kuwajibika kwa kuandaa hiyo mifumo tajwa,bhaasi unakomaza tatizo ambalo litakigharimu uzao wako,utawapa taabu sana,afu ni kosa kwa Mwenyezi Mungu pia,we amekupa afya njema,amekupa uhai,AKILI KICHWANI si mwendawazimu wala chizi kwamba ukapumzike milembe lah!Sasa kwa nini wewe uwe vivu,lizito,zembe,zubevu dhambi hizo.
Haijarishi umeajiriwa au umejiajiri we wajibika tuu kwaajili yako na kwa wengine utakuja jikuta unatoka kundi moja kwenda jingine yaani zile responsibilities kwa jamii yako utajikuta tuu zinakulazimu either uajiriwe au uajiri akili yako!
Ukimudu kula kulala kuvaaa usijicheleweshe nenda mbele zaidi mudu kulisha kuvisha na kufurahisha wengine iwe kwa kusomesha yatima,kugharamia matibabu ya watu wenye mahitaji,au kugharamia miradi ya huduma za jamii kule vijijini ambapo hapo utakuwa unaisaidia serikali kutekeleza majukumu yake.Mungu ana nafasi yake usiache kuyanyosha mapito yako, akili yako na matendo yako vinginevo bila hilo la mwisho utakuwa unajaribu kupaka rangi upepo!