Na hata huyo Kiranga si kwamba haamini Mungu kutokana na hizo sababu anazotumia humu kujengea hoja,hivyo hata wewe ukijaribu kujiweka nafasi ya kupinga uwepo wa Mungu pia utaona mapungufu ya huo msimamo.
Kama ingekuwa hoja za wapinga uwepo wa Mungu ndizo hasa sababu zenye kuwafanya wasiamini uwepo wa Mungu basi isingewezekana miongoni mwao wapinga Mungu kuja kuamini uwepo wa Mungu.
Chukua mfano mtu ambaye haamini Mungu na kusema hakuna uthibitisho wa uwepo wa Mungu halafu uje kusikia mtu huyo amekuja kuamini Mungu,hapo ndio utagundua kinachowafanya wasiamini Mungu ni tofauti na sababu wanazotoa.
Mshana Jr aliwahi kusema Kiranga ana mambo tu ambayo hajakubaliana nayo kwenye dini yake. Hata mie nakubaliana na hilo kwa sababu wengi wao hawa wapinga Mungu matatizo yao huanzia kwenye dini zao na badala kutafuta majibu matokeo yake ndio huangukia kwenye upagani.