detective mfaume
Member
- Dec 23, 2016
- 31
- 69
Kumekua na mvutano wa muda mrefu kati ya wanazuoni juu ya uhalali wa sheria za kimataifa kuitwa ama “Sheria za kimataifa” au ni “Kanuni za kimataifa.” Mvutano huu ni wakihoja ambao haujawahi kua na suluhisho la moja kwa moja.
Miongoni mwa sifa kuu za sheria ni ulazima wa sheria kufuatwa, kinyume na hivyo, huvutia adhabu fulani. Sheria ikivunjwa matokeo yake hua ni adhabu kwa alieivunja. Na ili hili likamilike ni lazima pawe na msimamizi wa sheria au chombo maalumu kinacho simamia matakwa ya sheria. Bila kusahau chombo kinacho amua kutendeka au kutotendeka kwa kosa au uvunjwaji wa sheria husika. Sifa hizi hufanya sheria itofautiane na kanuni au taratibu, ambazo binadamu hijiwekea kama muongozo.
Mataifa yenye nguvu yamekua yakivunja sheria za kimataifa mara kadha wa kadha bila hatua stahiki kuchukuliwa kutokana na ushawishi wa mataifa hayo duniani. Leo nitazungumzia marekani pekee, tupate kujifunza na mwisho kabisa kujiuliza, tuziite ama sheria za kimataifa au kanuni za kimataifa.
Tangu kuanzishwa rasmi kwa mahakama kuu ya umoja wa matifa ya haki (ICJ) mwaka 1946 marekani imeitwa kujibu mashauri 13. Yote yakiwa ni malalamiko ya ukiukwaji wa sheria za kimataifa. Ni jambo zuri na ni matakwa ya sheria kufikisha migogoro ya ukiukwaji wa sheria katika mahakama hii. Tatizo ni kwamba hakuna namna yoyote utekelezaji wa maamuzi yanayotolewa na mahaka hii yanaweza kusimamiwa.
Kuingilia na kutumia nguvu ndani ya mataifa mengine: ni muda mrefu sasa marekani imekua ikiingilia na kutumia nguvu ndani ya mataifa mengine kama Syria. Mwanazuoni Michael Ratner ameita kitendo hiki kama “Illegal use of force and crimes of aggression.” Ni uhalifu wa kivita na ni aina ya uhalifu ambao German ilishitakiwa katika mashitaka ya Nuremberg mwaka 1945.
Mataifa mengi yameingilia vita ya Syria wengine wakisaidia serikali kama Urusi, huku wengine wakisaidia waasi, kama Marekani, Ufaransa, Uingereza na Saudi Arabia. Huku sababu inayotumika kuingia ni kupambana na kundi la dola ya kiislamu, ISIS.
Katika miaka ya 1980s Marekani kupitia shirika lake la ujasusi wan je, CIA ilisaidia waasi katika harakati za kutaka kupindua serikali ya Nicaragua. Marekani ilitoa msaada wa kifedha, mafunzo na silaha kwa waasi. Kufuatia tukio hili Nicaragua ilipeleka shauri katika mahakama kuu ya umoja wa mataifa (ICJ) kuishutumu marekani kwa uvunjaji wa sheria zakimataifa na kudai fidia ya kiasi cha dola bilioni 17. 1986 ICJ ilitoa hukumu juu ya kesi hii, na ikiikuta Marekani na hatia ya ukiukwaji mkubwa wa sheria zakimataifa. Sheria za kimataifa zinakataza kitendo cha nchi moja kuingilia nchi nyinginge.
Baada ya kukutwa na hatia, marekani ilijitoa katika kuisaidia mahakama ya umoja wa mataifa. Na kwakua marekani ni “permanent member” wa baraza la usalama la umoja wa mataifa, hadi leo hii Nicaragua haijapata fidia yoyote.
Mashambulizi kwa raia: mwaka 1989 marekani ilirusha makombora na kulipua ndege ya raia na kuaa watu 290. Ndege hii ya Iran ilijulikana kama “Iran Air Flight 655” na ilikua katika anga la Iran. Iran ilifungua shauri katika mahakama ya umoja wa mataifa. Lakini mwaka 1996 marekani na Iran ziliingia makubaliano. Marekani ilikubali kulipa kiasi cha dola milioni 61 kwa familia zilizopoteza wapendwa wao katika shambulio. Mpaka leo hii marekani haijawahi kuomba msamaha kwa tukio hili.
Ukiukwaji wa sheria zakidiplomasia: mwaka 1999 marekani ilihukumu adhabu ya kifo kwa wajerumani wawili bila kujulisha ubalozi wa ujerumani. Hukumu hii ilitokana na mauaji yaliojitokeza katika unyang`anyi wakutumia silaha uliofanyika bank, mwaka 1982. Katika shauri watuhumiwa hawakujulishwa haki yao ya msingi yakupata msaada kutoka katika balozi yao. 2001 mahakama ya umoja wa mataifa ilitoa uamuzi kua marekani ilivunja mkataba wa umoja wa mataifa “Vienna Convention on Consular Relation. Marekani iliahidi kutorudia tena.
Mwaka 2003 Mexico ilifungua shauri kuishitaki marekani kuvunja vipengele vilevile katika mkataba wa Vienna. Marekani ilikamata, kushitaki na kuhukumu adhabu ya kifo wamexico 54 bila ubalozi wa mexico kujua. Mahakama ya umoja wa mataifa kwa mara nyingine ilikuta marekani na hatia ya kuvunja mkataba wa kimataifa wa Vienna Convention on Consular Relation. ICJ iliitaka marekani kupitia upya mashauri na upatikanaji wa hatia wa mwamexico hawa na kuhakikisha kitu kama hiki hakitokei tena.
Badala yake marekani ilijitoa katika kipengele cha mkataba wa Vienna kinachohitaji marekani kufuata matakwa ya mahakama ya umoja wa mataifa.
Mashambulizi ya ndege zisizo na rubani katika sehemu mbalimbali duniani yanayofanywa na Marekani, ni ukiukwaji mkubwa wa sheria za kimataifa. Katika kile kinachoitwa vita dhidi ya ugaidi, marekani imekua ikituma ndege zisizo na rubani kulipua maeneo kadha wa kadha katika nchi za mashariki ya kati, kama Syria na Iraq. Mashambulizi haya yanalenga mpaka raia wa kawaida wasio na hatia. Haya yote ni matumizi ya nguvu isio ya kisheria chini ya sheria za umoja wa mataifa.
Ukiukwaji wa sheria za Anga: Sheria zakimataifa zinatoa mamlaka na haki kwa kila nchi juu ya anga lake na matumizi yake. Marekani imekua ikivunja sheria hizi kwakuingilia anga za nchi nyingne bila ruhusa ya nchi husika. Mfano mzuri ni Syria, ambapo marekani imekua ikituma ndege zakivita bila ruhusa. Ndege hizi zinalenga kushambulia kundi la kiislamu la ISIS, kwa lengo lakuzuia ugaidi, lakini huenda zaidi mpaka kushambulia wanajeshi wa Syria.
Utesaji na ukiukaji wa haki za binadamu: katika vita dhidi ya ugaidi duniani marekani imekua ikikamata kutesa na kuua watuhumiwa wa ugaidi katika sehemu zinazojulikama kama black sites. Mateso hufanyika ili watuhumiwa kukiri makosa. Kitendo hiki ni kinyume cha sheria za kimataifa zinazo kataza vitendo visivyo vya ubinadamu ikiwemo utesaji wa watuhumiwa.
Yapo mengi yanayofanywa na mataifa yenye nguvu kama marekani ambayo ni ukiukwaji wa sheria za kimataifa, lakini katika Makala hii nimeamua kuchagua matukio machache ambayo yapo katika historia huku mengine yakiendelea. Labda tunaweza kujiuliza, kuhusu tukio la mwanzoni mwa mwaka huu, marekani kumuua General Qassem Suleiman, katika ardhi ya Iraq kwa kigezo cha tishio la mipango ya mashambulizi , je ni ukiukwaji ya sheria za kimataifa? Hasa mkataba wa umoja wa mataifa unaokataza matumizi ya nguvu ndani au dhidi ya taifa lingine, isipokua kama kitendo hicho kitakua ni chakujilinda dhidi ya shambulio la moja kwa moja.
Na;
Mfaume Hassan
11 March 2020
mfaumehassan@gmail.com
Sent using Jamii Forums mobile app