Ukiwa barabarani, kuwa makini usije ukagongana na wanaotembea vichwa vimeinama kwenye simu mkononi

Bob Manson

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2021
Posts
4,158
Reaction score
7,787
Ukiwa barabarani, kuwa makini usije ukagongana na hawa, wakitembea vichwa vimeinama na simu mkononi. Wakitembea mbele hawaoni, wengine wanaishia mitaroni, wanakoswa kugongwa na magari.

Ukiwa barabarani, chukua tahadhari dhidi ya viumbe hivi hatari, kwani macho yao muda wote yapo kwenye vioo vya simu zao, vidole vyao vinaandika jumbe huku miguu yao inatembea.

Ukiwa barabarani na usipo chukua tahadhari, watakuvamia uso kwa uso hata kukuumiza, hawajali wapo eneo gani notification ikiingia lazima wafungue.

Ukiwa barabarani, kuwa makini na viumbe hivi hatari.
 
Ukiwa barabarani, kuwa makini usije ukagongana na hawa, wakitembea vichwa vimeinama na simu mkononi. Wakitembea mbele hawaoni, wengine wanaishia mitaroni, wanakoswa kugongwa na magari.

Ukiwa barabarani, chukua tahadhari dhidi ya viumbe hivi hatari, kwani macho yao muda wote yapo kwenye vioo vya simu zao, vidole vyao vinaandika jumbe huku miguu yao inatembea.

Ukiwa barabarani na usipo chukua tahadhari, watakuvamia uso kwa uso hata kukuumiza, hawajali wapo eneo gani notification ikiingia lazima wafungue.

Ukiwa barabarani, kuwa makini na viumbe hivi hatari..
Yaani utafikiri hafiki anakoenda na hakuna mitandao!
 
Hata mtembea kwa miguu na yeye inabidi afuate sheria za barabarani na si muendesha chombo cha moto peke yake.
 
Mimi nishawatia sana hasara hawa wajinga, namkwepa kidogo halafu nampiga kibega kiaina ule mkono ulioshika simu inakwenda chini halafu najifanya niko bize anashindwa aanzie wapi kuniuliza
 
Hao ndo huwa wanaibiwa town wanabaki kulalamika........

Afuu kuna wale ambao wana makoti yenye mifuko, au pochi Lakini simu wanashika mkononi tu kama prestige hao nao tuwafanyaje wakuu?
 
Ukiwa barabarani, chukua tahadhari dhidi ya viumbe hivi hatari, kwani macho yao muda wote yapo kwenye vioo vya simu zao, vidole vyao vinaandika jumbe huku miguu yao inatembea
Huwa nawanyoosha mabega,silei ujinga.
 
Hao ndo huwa wanaibiwa town wanabaki kulalamika........

Afuu kuna wale ambao wana makoti yenye mifuko, au pochi Lakini simu wanashika mkononi tu kama prestige hao nao tuwafanyaje wakuu?
Hao wanataka tuone sim zao zina camera ya macho matatu, wakiweka mifukoni hatutaona
 
Mimi nishawatia sana hasara hawa wajinga, namkwepa kidogo halafu nampiga kibega kiaina ule mkono ulioshika simu inakwenda chini halafu najifanya niko bize anashindwa aanzie wapi kuniuliza
Wengine hawana cha maana wanancho fanya kwenye simu ila siku muda wote zipo mkononi
 
Back
Top Bottom