Uchaguzi 2020 Ukiwa huna mipango ya ushindi ni vyema usipoteze muda wako kugombea uongozi Oktoba 2020

Uchaguzi 2020 Ukiwa huna mipango ya ushindi ni vyema usipoteze muda wako kugombea uongozi Oktoba 2020

Zee la kitaa

JF-Expert Member
Joined
Oct 25, 2017
Posts
403
Reaction score
211
Nimekuwa nikifuatiliia watia nia wengi walioanza kujitokeza na kufanya tathmini kidogo nimegundua wengi hawana mipango madhubuti ya kuwakomboa wananchi katika changamoto nyingi wanazokumbana nazo.

Wengine wanaona kama urais, ubunge na udiwani kama njia nyepesi ya kujipatia vipato. Wananchi wengi wamepata uelewa kuhusu nini wanataka na kiongozi wa aina gani wanamtaka.

Wananchi wanataka kiongozi atakayejibidiisha katika kutatua changamoto zinazowakabili regardless chama anachotoka. Kiongozi mwenye maono kwa taifa na jamii inayomzunguka.

Kiongozi asiyekuwa na makandokando ya kibepari na kiongozi anayetambua Tanzania ndio taifa lake na yuko tayari kupoteza uhai wake kwa ajili ya taifa lake.

Hivyo kwa kuangalia hayo utatambua wengi wanaotia nia wanashida na kukosa vigezo vya msingi. Vigezo vingine unaweza kuongeza wewe.

Naomba kuwasilisha
 
Siasa nisehemu ya ulaji ukombozi unapshwa ujikomboe wewe mwenyewe siyo kumtegemea mwanasiasa.
 
Back
Top Bottom