Nasema ninachokijua, nimeishi Zanzibar na kuona Wachagga walivyowekeza kule, vilabu vingi na maduka na biashara nyingi nyingi akina Mangi, nimetembelea mikoa mingi Tanzania, hao hao Wachagga unawakuta kote huko na lafudhi zao zile.
Hapa Nairobi jirani wangu Mchagga ameweka bonge la apartments tena za kifahari, kwa kifupi ukiwa mchapa kazi usie mzembe utapokewa kote. Lakini kama wewe mzembe wa kulialia, dunia itakutupia nje.
Nchi yetu hii ipo vizuri kiuchumi kwa sababu huwa tumewakaribisha wageni wawekeze, Wasomali walipopigana kwao huko, matajiri walikuja na mihela na kuwekeza kwa kwenda mbele, mabwenyenye wa Sudan Kusini ndio usipime.......
Mtaani kwangu hapa vinyozi vingi vinamilikiwa na Wanyarwanda.....punguzeni kulialia.
Rais Uhuru alishasema hataki kuskia wageni haswa wa EAC wanazuiwa kwa chochote, yaani unaruhusiwa hata kumiliki kiwanja, ushindwe mwenyewe. Ukiona mtu anazuiwa ujue kuna kitu nyuma ya pazia sio bure. Tunawahitaji sana wawekezaji, waje na hela kama zote....hii ni nchi ya kibepari hatuna hizo pumba za ujamaa.