Ni kweli hilo huwa lipo lakini ni ufinyu wa ufahamu wa hao wanaokuangalia ,lakini basi ni vema jamii ikatambua kuwa vvu au aina yeyote ya mabaka si ukimwi wala haimaanishi kuwa umeambukizwa kwani yaweza kuwa ni matokeo ya mojawapo ya mabmbo yafuatayo ;-
1.Ugonjwa wa ngozi ambao umesababiswa na upungufu wa chembe chembe fulani mwilini.
2.Tatizo au adhari za matumizi ya dawa wakati wa matibabu fulani (side effect) chukua mfano wa
dawa za malaria zilipobadilishwa wengi walipata ulemavu mfano mzuri ni zile SP.
3.Sumu inayopatikana ndani ya chakula na haishabihiani na chembe chembe zilizopo mwili.Hili wengi
huwa wanasema ni allegy.Unakula chakula ambacho kinaudhuru mwili bila mwenyewe kujitambua.
Hayo ni baadhi tu ya mambo ambayo yanasababisha hii hali .Ingawa basi yawezekana ikawa kama wanavyotafsiri lakini hiyo haimaanishi atengwe au aonekane yupo tofauti.Kikubwa ni kwanza mgonjwa mwenyewe yaani mwenye mabaka ajitambue na kujikubali huku akiwa anatafuta ,ufumbuzi wa hilo tatizo hilo na pia jamii iweze kutambua kuwa si kwamba naye kapenda hiyo hali lakini imemtokea .
Nategemea sana kwa wana JF kuwa wanamsaada mkubwa endapo watakutana na mtu au watu wenye tatizo kama hili.na kwa maoni yangu ,endapo kuna yeyote anayeweza kujua au kutoa tiba ya hilo tatizo ,amsaidie / kuwasidia mtu/watu hao endapo wanapatikana.