Ukiwa na Milioni 10 kijijini mfano Kahama, Nzega, Igunga na Geita fanya biashara ifuatayo ukimtegemea Mungu

If u want to succeed go against the norms... Time is money!
Hizi biashara za kuzika pesa kwa miez unakuja kupata faida km hyo ni bora kukaa chini ni kufirikia zingine! Ni maoni tu hata hvyo!
Ni kweli. Milioni 10, kupata laki 6 kwa mwezi bado siyo akili nzuri. Kuna dili nyingi za kuzungusha hiyo hela, ukapata pakubwa.
 
Weka dili mkuu.

Ila nadhani kwa mtu ambaye hana dili kubwa na hajapata bora awekeze huko kuliko kukaa nayo akisubiri dili kubwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Nilitumia milioni 5, nikanenepesha ngombe maeneo hayohayo mara mbili( miezi 6) nikazalisha 7M , mtaji ukafika 12M . Hizo 12M nikahama nikawekeza Mradi wa ng'ombe wa Maziwa. Nimemwachia kijana wangu, anazalisha lita 150- 200 za Maziwa kwa siku!!!! Lita moja anauza 1300- 1500 Tsh.
Mwaka jana mwishoni aliniambia ana mpango wa kuagiza mashine za kuchakata mazao ya maziwa baada ya kununua eneo na kugharamia miundombinu mingine (gharama zote hizo siyo chini ya 30- 40 M).
Asante.
 
Kumbe ng'ombe wa maziwa wako vizuri kwa kuendesha maisha
Hongera mkuu
 
biashara ya kwenye keyboard huwa ni rahisi sana......sasa kwa mfano gharama ya kuyahifadhi ni kiasi gani??tuanzie hapo
 
mkuu nakuomba chemba
 
Kuna utofauti Mkubwa sana wa Kusimuliwa jambo unalotaka kufanya na kulifanya ukaona uhalisia.

Kurudishwa nyuma Kimaendeleo moja ya sababu kubwa na jinsi jamaii inayokuzunguka inavyokukatisha tamaa.

Mambo yasiyo eleweka na shauri zenye kutisha na hata nyakati zingine kuficha kweli zilizopo ili tu watu wasinyanyuke kiuchumi.

Nakumbuka nyakati za Shule..mtu anayekutangulia anakutishia wee sikia Logarithm topic ngumu mno.

Lakini kama ukawa na akili timamu unasema ni kwake si kwangu.Kushindwa kwako kusiwe kigezo cha kumfanya anayetaka kujaribu au kupambana na Maisha kuwa wewe ndio Mwisho.

Tunaweza kufanya kitu kile kile wote ila sababu za kushindwa ni kutaka kufanana na kushindwa kujua utofauti wa fikra zetu.

Huwa najifunza sana kwa Wacheza Mpira hawa wakubwa huko kwa wenzetu.

Unaona wanakotokea na wanavyokuwa baadae.

Usikate tamaa kwa kuwa tu MIMI nimeshindwa basi wewe Ushindwe.Fedha inahitaji NIDHAMU ya hali ya juu sana na RECORDS.

Kuwa na hakika kwa unachotaka kufanya na amini kuwa kuna faida na Hasara na zote hutofautiana.
 
Mahindi biashara ya kuchekesha sana... Mwakajana mwez kama huu yalishuka yakauzwa being ya pumba mwaka huu yanepanda yanauzwa bei ya dhahabu
 
Mbona hujazungumza gharama za kuhifadhi kwa miezi hiyo 6 ya kungokea bei nzuri ? Na pia kwenye elfu 2 ya costs ulizotaja sidhani kama zina uhalisia . Maana kuna gharama za kukusanya , magunia ya kuhifadhia / viroba , gharama za usafirishaji , ushuru na gharama nyinginezo chache zisizoepukika ( Huwa mnaita dharura ) . Nafikiri wazo ni zuri ila limepungukiwa na uhalisia kwa kiasi fulani .
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…