Ukiwa na tabia hizi, jiandae kuwa middle class na kuteseka ki uchumi!

Nyumba gani ya kupanga unaweza fuga kuku na kitimoto? Mie nkipata kazi najenga nyumba then naanza mradi sio kuishia kutajirisha wenye nyumba! Sasa mtu unanyumba za kupanga afu waish nyumba ya kupanga inakuwaje hyo?
 
very funny.sijaelewa unataka watu walale wapi? kazini,bar au guest? unataka mtu akae kwenye nyumba yakupanga gharama yake kwa mwaka kwa nyumba yenye hadhi ya mtu kuishi plus mazingira yanayoruhusu akili kupumzika baada ya kazi ngumu za mchana? huwezi kuwa serious bila ya nyumba tunaishi wapi labda? unataka baba wa familia ya watoto sita apange chumba kimoja?
 
umeona eeh!! kuna watu kwanza mshahara wao mwezi mmoja tu ni gharama ya vitz mpya. kwanini asijivutie zake usafiri huku anajipanga zaidi na life.

Mkuu apa tunaangalia asilimia kubwa ya watu hao wanaolipwa mshahara mamilion apa hayawahusu ukitaka kuwaiga sawa
 

Sijui labda we umewekeza kwe kamtaji gani ka kukuvimbisha kichwa kudiss wengine......watu wanaamua kuinvest kwe nyumba koz its atleast a security atakayo kuwa nayo mambo yasipokaa poa....tunajaribu sana muiga robert kiwasaki tunasahau jamaa ukiacha na mifano yake yoote ye kapiga ela kwe kuandika vitabu tu.....bora warren buffet namkubali..
 
una nyumba mbili na bado una shida ya kiuchumi. ungekuwa umepanga hali yako ingekuwa mbaya zaidi. waone consultants.
aisee hata mimi niliteseka sana infact i have 3 house but maisha yalikuwa magumu na nilikuwa restless mpk nyumba moja nilipoigeuza lodging house seriously am relaxing do that my friend,rents is hopeless money and stupidity do that goodwish!
 
sidhani kama kuna ukweli, maisha ni kujipanga na kupanga ni kuchagua. nyumba na gari nayo ni mahitaji ya msingi sana tu ya kuanza nayo kama hukuwa navyo na haijalishi ununue vya kwanza au vya mwisho, jitihada binafsi ndio muhimu zaidi

Watu wanataka ku simplify mambo sana na kutupa formula kama maisha ni sawa, wote tuko sawa na tunataka vitu sawa.

Wengine hawataki utajiri wa mali, bali utajiri wa experiences, ikiwa ni pamoja na kutulia sehemu nzuri na familia. Sehemu nzuri hizi zinaisha na kuwa adimu kadiri miaka inavyoenda.

Utamwambiaje mtu asijenge anapoona inafaa na panafaa?

Especially kama anaweza kuuza nyumba muda wowote, na nyumba ni asset inayoweza kutumika kama store of value?

I mean I get the idea that, if you are in a high yield business, one that could guarantee you a quick %25 + turnover profit, if you have a hundred million shillings, and you are a young man starting a family, you can afford to rent and invest your money to maximize money circulation and profit generation.

But how many people are in that position?

How many people have the requisite business acumen and are suitably positioned to be swift businesspeople without adverse trade offs?

Kuna kaka mmoja namjua, mtu wa mitkas sana. Alifanya mambo yake akapiga hela kubwa. Akajenga Mbezi Beach na kuendelea kuzungusha. Baadaye mambo hayakumuendea vizuri. Kauza nyumba yake a couple hundred million shillings, ka downsize, katumia hela kurudi kwenye biashara.

Pengine asingejenga hata hizo zilizomrudisha kwenye biashara asingekuwa nazo.

Kila mtu anahitaji sehemu ya kukaa. Sehemu kama bongo haijaendelea kimakazi useme renters wana specific advantage over owners. Owners huko hawana tax disadvantage kama zetu baadhi ya owners in the west, to my knowledge.

Kutoa ushauri blanket bila ku acknowledge kwamba at least different people may need different solutions ni irresponsible
 
Kama ukiwa mpangaji kwa mtu......... huoni kama ukijenga kwako mapema hizo kodi zitaenda kufanya mengine...... mimi naona fanya mambo ya kukujijenga kama kijana huku ukizingatia suala zima la matumizi mazuri ya rasilimali zako kama pesa na kadhalika........
 
Husninyo,

Wanafananisha Bongo na mbele

There some parts in this world can be comfortable kuishi maishi yako yote kwenye apartments sio tz unless umepata zile nyumba za Mchechu kwa bei poa na 'ujanja ujanja' hulipii umeme na maji

Watumie akili kidogo, wanalinganisha sehemu watu wananunua nyumba na tz unajenga. Bunju,Goba,Chanika kwako ni salama kwa watoto kuliko Kino na Sinza kwenye nyumba za kupanga
 
Last edited by a moderator:

Mkuu ur wrong...Nyumba nimuhimu kuliko kitu chochote duniani...Gari sio muhimu sana au wewe unaweza kulala nje?
 
aisee hata mimi niliteseka sana infact i have 3 house but maisha yalikuwa magumu na nilikuwa restless mpk nyumba moja nilipoigeuza lodging house seriously am relaxing do that my friend,rents is hopeless money and stupidity do that goodwish!

mkuu kujenga nyumba ya m60 afu utegemee urudishe pesa zako thru kodi ni UKICHaa
 

waeleze mkuu, tena hii kauli yao ya kusema ukijenga nyumba sawa na kufukia hela ardhini sijui wameipata wapi. nyumba unayojenga leo baada ya miaka kumi ukitaka kuiuza thamani yake haiwezi kuwa ile ile. watu walikuwa na nyumba za kawaida tu kariakoo na wameziuza pesa ndefu na wengine mpaka leo wanasumbuliwa na wateja wauuze hata kwa mabilioni. ushauri wake mzuri ila kweli hauwezi kuwa sawa kwa watu wote na ingebidi aliseme hilo.
 
watu wanafikiri wote apa tunalipwa laki saba saba....wengine iyo ni airtime ya mwezi mzima!!!atafute helaaa

Nakubaliana na wewe kabisa, hasa kwa kuzingatia jina lako, umeenda dom msimu huu?
 
umeona eeeh!! naskia huko mbele kumiliki kiwanja tu sio rahisi, sembuse huku tz maeneo kibao yamejaa na waweza lipia hata kwa installements. tena nyumba ni investment nzuri sana maana mambo yakiwa magumu licha ya kuuza unaenda zako kupanga vyumba viwili huku unapokea kodi ya nyumba nzima.
 

Nilikuwa nasoma article moja last week. Imefanya a "renters vs. owners" comparison, based on North America data if memory serves. Wanasema renters wana advantage in the first four years, baada ya hapo advantage inayeyuka na kuwa disadvantage, unakuwa unalipa kodi kama mortgage tu.

Speaking of mortgages, huyu anayetoa ushauri ana assume kwamba mtu atatoa hela yake mfukoni kujenga. Wakati watu siku hizi wanachukua mortgages.

Na unaweza kuchukua mortgage kujenga nyumba, ukajenga nyumba, ukaonesha stability kwamba unalipa mkopo vizuri na una hati ya umiliki nyumba inayoweza kutumika kama collateral, ukaomba mkopo mkubwa zaidi na kufanya biashara kubwa zaidi.

Nenda kuomba mkopo kwa kutumia a rented apartment/ house kama collateral uone.

Ndiyo maana nikasema ushauri huu tuliopewa unaweza kuwa sawa kwa baadhi ya watu na usiwe sawa kwa baadhi, kutegemea na specific za situation.
 
Last edited by a moderator:
Kwa tanzania kwa mfano watu wengi tunaonaona mafanikio ni gari la kutembelea wkt walioelimika mafanikio ni uwekezaji wa aina nyingi na wenye faida "money circulation" ndo hitaji la msingi ktk kumiliki pesa nyingi yani hii ni sawa na mtu anayeajiriwa na kuchekelea huku akisahau yupo pale ili kutimiza malengo ya mjasiliamali aliyemwajiri yeye
 
Ushauri umetolewa kwa mazingira hasa ya tanzania na umewalenga vijana ambapo kisingi vijana wengi Tz ndo wale wanaosubiri ccm iwaletee au chadema iwape maendeleo hata exposure tu za mikopo na ubunifu hakuna



 
1. Kutokukua kiuchumi zaidi ya kubakia kama mlaji wa mwisho(final consumer)
2.kutokuenenda na changamoto za mabadiliko ktk dunia ya ushindani
3.kua na ajira ya direct way ambayo utanyenyekea milele waajiri wako
4.kutojitosheleza kimahitaji wewe na familia yako kwa ujumla



Kuna UBAYA gani kuwa MIDDLE CLASS?
 
Mkuu ur wrong...Nyumba nimuhimu kuliko kitu chochote duniani...Gari sio muhimu sana au wewe unaweza kulala nje?

Nyumba ni muhimu lakini inakula pesa nyingi na muda mrefu hasa kwa pesa za mishahara, hiyo pesa ingeingia kwenye biashara zingine ingekuwa zaidi ya m4 kwa mwezi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…