Ukiwa na tabia hizi jua mwenzio anakereka!

Mtambuzi

Platinum Member
Joined
Oct 29, 2008
Posts
8,809
Reaction score
15,421
Watu wengi wanapozungumzia kuvunjika kwa ndoa au uhusiano, sababu zinazojitokeza sana au kutajwa ni zile za ulevi, kutoka nje ya ndoa, kipato, uchafu, na mengine ya aina hiyo, lakini wanasahau kuwa kuna baadhi ya tabia zenye kukera ambazo kama zisipoangaliwa kwa makini zinaweza kuipeleka ndoa au uhusiano shimoni:

Nitataja baadhi ya tabia hizo kwa uchache ili nisiwachoshe:
1. Kujilinda- ni kitendo cha mwanandoa kutopenda kupingwa, kwa namna yoyote, hata pale inapoonekana dhahiri hayuko sahihi, atatumia muda mwingi kujitetea na kutoa mifano chungu mzima isiyo na kichwa wala miguu.

2. Kutofurahia ukimya- mwanandoa asiyefurahiya ukimya ni yule ambaye mdomo wake unamuwasha wakati wote anapenda kuongea tu, na wakati mwingine huongea utumbo mtupu. Mara nyingi watu wa aina hii hupoteza kumbukumbu ya kile walichosema au walichozungumza muda mfupi ulipita.

3. Utani ulopita kiasi- uchekeshaji ni mzuri sana katika kuboresha ndoa au uhusiano na hujenga afya kwa wanandoa unapotumiwa vizuri. Lakini pale utani unapozidi unakuwa ni kero kwa mwenzako. Utani unakuwa mzuri iwapo utatolewa kwa muda muafaka. Kuna wakati unaweza kukuta mwanandoa anatoa utani wenye kushusha na kutweza bila kujali hisia za mwenzake hii ni hatari sana katika ustawi wa ndoa. Kuna wakati unaweza kukuta mwanandoa roho yake iko juu juu pale wanapotembelewa na wageni maana anakuwa na wasiwasi kuwa mwenzake anaweza kumfanyia utani wa ajabu kabisa nakumuharibia siku na kumuabisha kwa wageni.

 
Uchafu.. na kutokua makini kwenye mipangilio ya vitu.
Unaweza kuja ukakuta kiatu juu ya friji(joking....) hasa kwa ile jinsia nyingine
 
Nimeipenda ila nahitaji zaidi maana zipo chache
 
kwa kweli ile kujilinda mie huwa siipendi zaidi, mtu kaona kabisa kakosa hata kukubali kosa hkuna ,mbish kupita kiasi....ni mengi sana hujaandika hapo , gubu nalo ni ishu ingine.thanks kwa kutukumbusha mtambuzi
 
Nimeipenda ila nahitaji zaidi maana zipo chache

Ni kweli, ndio maana nikasema nitazitaja chache ili nisije nikawachosha kwa kusoma maelezo marefu.......thread hii nitaiendeleza hapo nitakapopata muda, lakini pia nimewaachia wengine waweke kero zao, sikupenda nimalize kila kitu.............
 
Uchoyo, mie sipendi mtu choyo, awe mke au mume, hata wageni wakija ananuna, hii nahisi huwa namkwanza mwenza wako
 
Tafadhali toa maelezo zaidi juu ya hili GUBU sisi wa Bara hatulijui vizuri
Gubu analo mtu anayependa kulalamika tu, kila kitu yeye analalamika, hata akiona umeacha mlango wazi annaweza ongea masaa mawili, kila kitu yeye ni kulalamika na maneno hayaishi
 
Kutoa siri za ndani kwa wasiohusika/kwa watu wa nje
 
Nimekubali! Lakini pia kuna hili la ujuaji kiukweli linakera mno maana utakuta mtu anajifanya kujua kila kitu na kumwona mwenzake hakuna anachokijua na mwisho wa siku hujiona mwalimu au kiongozi anayestahili kumwongoza mwenzake kwenye kila jambo. Inaboa kupita kiasi!
 

unahitaji neema ya mungu kuwa na ndoa au mahusiano imara kwani hayp yote unayosema watu wanayafuata ila bado ndoa na mahusiano yao matatizo kutwa kukicha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…