Kwanza naomba nikupongeze kwa hatua kubwa ulio fikia.
Zaidi nikushauri uzingatie security, jitahidi kujua watoto wako wanacheza na watoto wa akina nani, jitahidi watoto wako wasipende kutoka/kucheza nje ya uzio wako.
Zingatia mambo ya kijamii inayo kuzunguka, ila usipende kupendwa na jirani zako hadi pale utakapo wajua vizuri tabia zao.
Nyumba mpya inaraha zake mkuu, ila ukisha hamia ndipo utaanza kuona kasoro zake na hapo ndipo utaanza kukosoa kwamba hapa na pale fundi alikosea na pengine ingekua hivi.
Ukihamia kwenye nyumba mpya, jitahidi pia fanya mpango uwe na usafiri wako mkuu.
Kwaleo naomba niishie hapa.