Unafiki juu ya kifo cha Ditto sitaki kabisa.Naamini kila mwanadamu atayaonja mauti na hili sina wasiwasi nalo.Nadhani Mungu sasa yuko upande wa watanzania wanaodhulumiwa haki za na baadhi ya watu wenye mamlaka ha TZ.
Kesi ya mauaji iliyokua ikimkabili mheshimiwa huyu ilipindishwa na watu wasiokua na akili mpaka kudiliki kupindisha sheria na kuanzisha vitu ambavyo havipo kabisa.Kimsingi kwa taaluma ya sheria ninayoijua mimi,hakuna kosa la kuua bila kukusudia lakini watu wasiomtanguliza Mungu wakaona ni vyema wawadanganye waTZ ili mtu wao muuaji atoke jela.Kuua bila kukusudia ni pale Jaji anpotoa hukumu ndio anaweza kuona kwamba kutokana na ushahidi uliotolewa mtuhumiwa aliuua bila kukusudia na sio katika process au ktk mwenendo wa mashitaka mtu anakurupuka eti huyu aliuua bila kukusudia how mwanasheria huyu alikula rushwa.
Kufa kwa JK sorry kufa kwa Ditto,ni majibu ya Mungu kwa kilio cha watanzani na mahabusu walioko magerezani kwa miaka dahari tena walioua kwa bahati mbaya kweli kuliko hata hii ya Ditto.
Sauti ya wengi ni sauti ya Mungu.Mliojua mnajua sheria mtajiju,mliokula njama za kumtoa Ditto mmeula wachuya,Yaani mambo yamewaendea kombo mbwa nyie.
Mimi siamini na sitaki kuamini kwamba mtu akifa na maovu yake yanakwisha huu ni UNAFIKI.Ditto ni mdhambi tu,kwa killing ya makusudi.
JK hili ni fundisho kubwa sana kwako,uliambiwa Lowasa hafai ukalazimisha lakini Mungu amekuchapa Kiboko,Ukasimamia uharamia wa Ditto Mungu amekuchapa kiboko kingine,Ukaambiwa Chenge hafai amejiuzulu hicho nancho ni kiboko kingine.Kuwa msikivu kwa vilio vya wananchi wako.Wewe sio mbabe hata kidogo,kumbukeni Mungu ndio yuko mbele yenu,fanyeni kazi kwa kumpendeza yeye na sio vinginevyo.