Nilikuwapo huko miaka ya 2007/2008... Ni kweli usemayo... sema Mto ukijaa kaa tayari kulala na mamba chumbani..:biggrin1:Nilipata kutembelea bonde la Kilombero(Ifakara) wakati fulani. Wakati wa msimu wa kilimo,kuna uhitaji mkubwa sana wa matrekta. Unakuta mtu mmoja ana oda ya kazi mpaka anachemsha. Yaani trekta linafanya kazi sana, wakulima wanalipa in-advance ili wapate huduma. Ukimaliza kulima trekta linageuka basi wakati wa masika, kumbuka huko mvua ni nyingi, kwa hiyo barabara hazipitiki.
Wakati wa mavuno, trekta linakuwa lori, kuna vijiji vina matatizo makubwa ya usafirishaji mazao. Jamani fursa za biashara ni nyingi mno.
Asante sana Malila, nakuunga nkono ni kweli kabisa shida ya matrecta bondeni kule ni kubwa mno! niliwahi kuoda kulimiwa nikakosa na nikapata hasara mwisho wa siku, kazi ni nyingi mno! niko kimya sana Bro, najipanga ile mambo yetu!!
Bila kusema uongo,inakwenda vizuri sana. Nilikwenda kule ili walau nipate shamba la kulima migomba.Wamekusikia mkuu. Hope nawe ile biz yako inaenda vyema
Nilikuwapo huko miaka ya 2007/2008... Ni kweli usemayo... sema Mto ukijaa kaa tayari kulala na mamba chumbani..:biggrin1:
Mimi na mamba damu damu, pale mkuranga walijichanganya wakaingia anga zangu nikawaitia Mzungu fulani, kawalamba wote hadi mayai yao. Hiyo nayo fursa nyingine.
Hahahaaa mkuu umenfraixha kwakwel