Itoye
JF-Expert Member
- Sep 29, 2017
- 531
- 1,023
Leo Tarehe Mosi September tumebakiwa na siku 56 ili tukawachague viongozi watakaotufaa kwa miaka mitano ijayo, kutokana na sera na ahadi ambazo tumezisikia hadi sasa kutoka kwa wagombea mbalimbali ni dhahiri kuna makundi mbalimbali ndani ya jamii ni muhimu sana kufanya maamuzi kwa kupima mustakabali wake huko tuendako:
Kama wewe ni mtumishi wa umma na unataka kuona malimbikizo ya mshahara wako yakilipwa, unataka kuona ukipanda daraja na mshahara kwa mujibu wa sheria basi wa kumchagua ni Tundu A Lissu.
Kama wewe ulikuwa mtumishi na umelitumikia Taifa kwa weledi lkn ukaondoshwa bila hata kifuta machozi kwa sababu tu ya vyeti, wa kukufuta machozi ili uufurahie uzee wako na jasho lako kwa Taifa hili ni Tundu A Lissu.
Kama wewe una ndugu aliyekumbwa na madhira ya vyeti akaondolewa bila kifuta machozi, mfaraji amejitokeza usiache kufanya maamuzi kwa ajili ya ndugu yako ni Tundu A Lissu.
Kama wewe ni Mkandarasi na umechoka kuona Miradi yote ikifanywa na Taasisi za Serikali, umechoka kuona mkitiwa ndani na watendaji wa Serikali hata pale ambapo makosa si ya kwenu au bila kusikilizwa, mtetezi halisi wa wanyonge ni Tundu A Lissu.
Kama wewe ni mfanyabiashara na umechoka kuonewa na mamlaka, umechoka kufilisiwa kama ndugu yetu Ntuze wa Kariakoo ambaye aliahidiwa fidia lkn mpaka leo anazungushwa, unataka ahueni ya utitiri wa kodi basi mtetezi ni Tundu A Lissu.
Kama wewe ni mwanafunzi wa elimu ya juu na unataka unafuu ktk kupata mkopo na baadae kulipa huo mkopo, Tundu A Lissu ndio mtu sahihi ameshasema 15% anaifuta 3% inarudi, usifanye makosa.
Kama wewe ni mnufaika wa mkopo wa elimu ya juu na unaumizwa na makato makubwa basi usijiulize mara mbili mbili, Tundu A Lissu ndiye mtu sahihi.
Kama wewe ni muhanga mwenzangu wa fao la kujitoa, Tundu Lissu ameshasema linarudi hakuna kusubiri hadi mtu azeeke ndio apate chake, tusifanye makosa.
Sote tunataka bima ya afya nafuu na tunayoweza kuimudu haijalishi uko kijijini au mjini na itakayokuwezesha kutibiwa hospitali yoyote ile sio bima inayoishia hospitali ya ngazi fulani au ugonjwa fulani tu, Tundu A Lissu amejipanga ktk hili.
Ajira, Ajira, Ajira na uchumi uliofunguka utakaowavutia wawekezaji wakubwa kutoka popote duniani na sio maelezo ya kuwa kuna maelfu ya viwanda vineanzishwa lkn vijana wanagangaika mitaani, Tundu A Lissu ndio jibu.
Uhuru, haki na Maendeleo kama umechoka na sheria kandamizi zinazominya uhuru wa mawazo, kama unataka kuona nchi ambayo kweli hakuna mtu aliye juu ya sheria kama unataka kuona nchi ambayo kika mtu endapo atafanya makosa anawajibishwa, kama unataka kuona "clear separation of powers" jibu ni Katiba Mpya na ni mtu mmoja tu hadi sasa amesema hiyo ni ajenda yake naye ni Tundu A Lissu.
Kama unataka kuona Commander in chief ambaye pia atakuwa Comforter in Chief basi ni Tundu A Lissu.
Usichague mtu kwa sababu tu atajenga barabara, reli, bandari, ndege, madaraja hayo ni mambo na mahitaji ya msingi ambayo serikali yoyote inayojielewa inapaswa kuyafanya na ndio maana tunalipa kodi, Baba bora hasifiwi kwa kuleta chakula nyumbani au kuhakikisha nyumba yake ni bora kwa ajili ya familia yake huo ni wajibu wake wa msingi kwa sababu alikubali mwenyewe jukumu la ubaba bali baba bora husifiwa pale anapoweka mazingira mazuri yanayohakikisha familia yake inaendelea na kustawi vizazi na vizazi vijavyo.
Mambo ni mengi lakini, Tundu A Lissu hadi sasa ametuonyesha njia na mwelekeo sahihi ambao kama Taifa tunapaswa kuelekea.