Jamani wanawake wote mliochangia humu mnanichanganya.Ni kitu gani kinakufanya uape kutoolewa na kijana mwenye watoto/mtoto?Karibu wote mnazungumzia rabsha ya mama wa watoto kuja na kukuharasi wakati unaishi na wanae,kweli kama hali hiyo ipo ni tatizo,lakini kuna kitu nakiona hapa kwenye kauli zenu japokuwa mnajaribu kukificha kwa kivuli cha sababu ya kusumbuliwa na mama wa watoto wa kuwazaa.Nilishawahi kujiuliza hivi inakuaje mwanamke anamtesa mtoto,tena mtoto wa mumewe anaempenda?Naanza kuupata ukweli mchungu.Ukiangalia,watoto wengi wanaoishi na mama wa kambo mama zao hawapo karibu hivyo zile rabsha za usumbufu wa mama zao hazipo,lakini asilimia 95 wanateswa,kwanini?Pia ni wanawake wachache wako tayari kumwachia mwanaume walieachana nae watoto,ukimuuliza sababu anasema wanae wataenda kuteseka!Wanawake hamuaminiani,huo ni ukweli,kwanini?Ni kama vile mna ugomvi toka muumbwe ndo maana ukiambiwa uishi na mtoto wa mwanamke mwenzio ni tatizo kubwa.Hata yule anaemsumbua mwenzake anaeishi na wanae nae ana tatizo hili hili,kuna kitu kinamkereketa moyoni kuona wanae wanalelewa na mwanamke mwingine!