Ukodishaji wa baisikeli za viwete (vilema)

Ukodishaji wa baisikeli za viwete (vilema)

IlangiKwetu

Member
Joined
Oct 9, 2014
Posts
85
Reaction score
33
Heshima mbele wadau,
Kama mjuavyo nimekuja kwa fuso la njegere hapa jijini juzi tuu, nikatokea hukoooo kijijini Madeke kwa wala Mbwa.
Back to the point ya msingi. Baada ya kushuka tuu nilikutana na hawa ndugu zetu walemavu. Barabarani wakiomba msaada kwa wasamaria wema wanaopita barabarani.
Nikatonywa kuwa kuna mjasiliamali kaona fursa kwa hawa wenzetu. Kanunua hivyo vibaiskeli vya kutosha halafu anavikodisha kwa hawa watu. Then jioni wanaleta salio kama wanavyofanya kwenye biashara ya botania.

Naomba kuthibitishiwa jambo hili. Sababu nimeuza shamba langu la miti huko na sitaki kurudi kijijini.
Na mimi nitumie hii fursa adhimu kujipatia kipato.

Nawasilisha.
 
Back
Top Bottom