SoC01 Ukoloni wa Kesho: Leo Ukoloni Mamboleo, 2150 Ukoloni Kamili tena

Stories of Change - 2021 Competition

Jetrudatabha

New Member
Joined
Jul 18, 2021
Posts
3
Reaction score
3
UTANGULIZI

Nina bahati ya kuandika Maneno haya, Maneno haya nitahadhali ya yajayo kama hatutoyaishi, Ninawaandikia vijana wote wa Tanzania Na Afrika kwa Ujumla Maneno haya yakawe Mwito wa Asubuhi kwa Vijana wote, Dhumuni kubwa la maneno haya nikuwaamsha vijana kuhusu

📌Serikali inaposema WAWEKEZAJI Pasi na shaka tunatakiwa kujifikiria sisi kwanza kama wawekezaji wazawa. Hivyo Maneno yangu Ni Mahususi kuwahamasisha vijana wawaze kuwa wawekezaji, vyovyote itakavyokuwa.

📌Kuliweka Taifa na Afrika mbele zaidi ya chochote hivyo nahamasisha Uzalendo.

📌Kutunza Rasilimali za Taifa kwa nguvu zetu zote na akili kwa ajili ya vizazi vijavyo.

📌Kuwatia Moyo vijana kwamba wakati wa kupanda mti ni sasa, wakati wakukuza teknlojia, sayansi, viwanda vyetu na uchumi wetu ni sasa, huu ndo mda wa kujipigania kama Taifa.

📌Ukweli Mchungu kwa vijana Misaada na mikopo ya Wazungu ni masimango, utumwa na manyanyoso kwetu Tuamini tusiamini!

MADA KUU

Tanzania na Afrika kwa Ujumla tunalilia wawekezaji kutoka nnje tujichunguze isije tokea ukoloni Miaka ya 2150.

Ndugu zangu kama wahenga wasemavyo kuwa historia huwa na tabia ya kujirudia rudia, Angalia Kati ya miaka 1880na 1912, Wazungu waligawana bara la Afrika, na nchi zote zikawa chini ya utawala wa Wazungu isipokuwa Liberian na Ethiopia, Mpaka waAfrika walipoanza kupigania uhuru wao na nchi za kwanza kujitawala upya katika Afrika ni nchi za Afrika ya Kusini zilizojiunga na kujiendesha wao wenyewe katika mwaka 1910, Misri, katika mwaka wa 1922walikuwa wanajiendesha wenyewe.

Madola mengi ya Afrika yalianza kupigania uhuru katika miaka ya baina ya 1950 na 1960 na Wazungu wakasalimu amri na kuanza kutoa uhuru.

Chanzo: Historia ya Afrika - Wikipedia, kamusi elezo huru

Miongoni mwa sababu zilizofanya wazungu kuja Afrika na hatimaye kututawala ni kutafuta.

✔️Madini

✔️Wafanyakazi

✔️Rasilimali za viwandani na

✔️Masoko kwa ajiri ya biashara zao.

Walipo ingia kwetu katika karne hiyo walitukuta na tamaduni zetu, na viwanda vyetu lakini baadae walitutawala nakutufanya kuwa watumwa na tegemezi, Wasiwasi ni kwamba zama hizo zaweza jirudia kama historia inavyosema sababu zilizowafanya Watu waulaya watutawale ndizo hizo ninazoziona leo nazo ni.

✔️Tunawakaribisha Wazungu, waarabu na wachina kwakutumia lugha ya kisasa kwamba ni WAWEKEZAJI WA KIGENI (External investors).Ni sahihi lakini hili linaturudisha nyuma karne ya 18 tulipowakaribisha kama wageni, mwekezaji anapokuja kwetu lazima tuingie makubaliano bila kusahau lazima aone yana manufaa kwake, wawekezaji hao ndio wanaoongoza uchumi hivyo huwa na maamuzi karibia kwa kila kitu, idadi ya wafanyakazi, mishahara, masoko, bei n.k ndio maana mpaka sasa tunaona kuna migogoro mingi baina ya wageni na wenyeji, Mfano Mgogoro uliotokea Afrika kusini siku za hivi karibuni, kwasababu aliyeshika makali ndio hula nyama sisemi kuwa hatupaswi kuwa na wawekezaji wa kigeni bali Tuamue kuanza kwanza sisi ili kuwe na hali ya 50/50 katika kumiliki uchumi, Fikilia ifikapo 2100 labda tuseme uchumi wa viwanda na masoko yamilikiwe na wachina au wahindi Tanzania tutakuwa na uwezo wa kumtunishia msuli nani? Mgeni siatakuwa na nguvu kuliko mwenyeji? Tuamue kumiliki uwekezaji kwa asilimia hata 60-70 halafu asilimia iliyobaki wawe wawekezaji wa kigeni.

✔️Dini zilizonanguvu ni kutoka ulaya nazo zinatumika kuwaaminisha wafuasi wake kuwa wazungu wana nguvu kuliko waafrika na zimezidi kujichimbia mizizi ndani ya Afrika. Dini zikitumika vibaya zitaturudisha nyuma lakini zikitumika vyema zitatupatia ukombozi wa kweli Rejea hapa namna dini zilivyotumika kudai uhuru




✔️Misaada, mikopo na fadhila tunazozipokea kutoka ulaya. Hii misaada haitusaidii bali inaendelea kutufanya tuwe masikini badala ya kuwa na mindset ya kujitegemea macho yetu yote tumeyaelekeza kwenye kusaidiwa, mbaya zaidi mashariti ya misaada hii ni makubwa, Afrika tumekuwa kama Dampo kila kibaya hutupwa kwetu viongozi wetu wamechoka kufikilia Labda kwasababu hunufaika na misaada hiyo.

✔️Afrika limekuwa Dampo la kupokea kila kitu kiwe kibaya au kizuri, kisiasa, kiuchumi na kiteknolojia.Hii hutokana na hali tuliyojiwekea kuwa vya Afrika havina thamani wala ubora, Afrika inapokea mashinikizo mengi kisiasa ambayo mwishowe huishia kuleta mitafaruku miongoni mwa waafrika hayo tumeyaona Libya na Sudani, Bila kuwa wamoja sisi wenyewe ni rahisi kwa Adui Kututawala.

✔️Waafrika wengi tunanunulika, sio wazalendo. Ni wachache walio na uwezo kama wa akina kinjekitile ngwale na akina chifu mkwaa walio tayari kufa kwa ajili ya nchi zao wengi wapo kwasababu ya Mali na vyeo, Kwasababu hizo chache nachelea kusema kuwa.

UKOLONI WA KARNE YA 18 UPO MBIONI.

Asante kwa Kusoma andiko hili

NAOMBA KURA YAKO.
 
Upvote 20
Link hiyo hapo

 
nice one 👍👍👍 tumekosa uzalendo, ndio maana tukipata cheo au nafasi kubwa serikalini tunaanza kujilimbikizia mali kwanza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…