Ukomavu wa Chadema

Ukomavu wa Chadema

otienolucas

New Member
Joined
May 6, 2024
Posts
1
Reaction score
1
Nimeamua kuandika kuhusu kuwepo na watu wawili viongozi wakuu wa chama kuonyesha nia kutaka kuwa wagombea urais kupitia chadema. Mimi hili jambo naliona kwa jicho la pili yaani chama kukua, pia kuwa na watu wenye ushawishi ndani na nje ya nchi.

Ili jambo linapaswa kupongezwa na sio kutiwa chumvi za kugombanisha viongozi hao na hata wanachama wanaowasapoti viongozi hao.

Viongozi hawa wawili wote ni Hazina na Tunu kwa taifa letu, ni watu wenye mchango mkubwa kwenye siasa za nchi hii. Mimi nadhani watu hawa wapewe moyo kuendeleza nia hiyo kwa njia nzuri isiyoweza kugawa chama. Ndani ya ccm wakati wa uchaguzi wa urais watu wengi ujitokeza na makundi yao, baada ya nomination makundi uzikwa na watu wote umpigia debe aliyeshinda. Tunaomba hata huku kwetu chadema wote wanaotaka kugombea wagombee atakayeshinda apewe sapoti nachama bila kupasuka.

Mimi siafiki kutafuta mgombea mpya nje au ndani ya chama na kuacha hawa majabali wawili yaani Tundu Antipas na mh Freeman Alikaeli mbowe.

Kuwa na makundi mawili yenye nguvu ndani ya chama kwa sasa yachukuliwe kama kukua kwa chama chetu. Hiki hakiwezi kuepukika kwenye siasa na chama kikubwa kama Chadema.

Tukatae neno tumuachie mtu fulani na mtu fulani asigombee,tukemee hila yoyote ya kutugawa.

By Otieno Lucas
 
ongeza jina la Heche yuko vizuri
 
Back
Top Bottom