Sir kitila
New Member
- Jul 29, 2022
- 1
- 0
ELIMU ni ujuzi anaoupata mtu ili umsaidie katika kujikomboa katika mazingira yake,na ujuzi unaweza kupatikana katika mifumo miwili ,mfumo rasmi na mfumo usio rasmi.
Hapa nchini Tanzania pamoja na kwamba tuna aina hizi za mifumo ya elimu lakini Bado mfumo unaotumika Sana ni mfumo rasmi ambao ndio msingi mkuu apa nchini kwetu kutoka darasa la awali mpaka chuo kikuu.
Ili, kujikomboa kifikira katika elimu hatuna budi kufanya yafutayo;-
Kubadili mtaala, hapa tunaona kuwa mtaala uliopo unamwandaa mtu katika hali ya kuwa tegemezi na siyo kujitegemea, wasomi wa leo wanawaza ajira kuliko kujiajiri ambapo hapa mtu hatumii ujuzi alioupata darasani kupambana na mazingira badala yake anakaa kusubiri ajira hali inayopelekea kuwa na upeo mfupi wa kufikiri
Kubadilisha mitizamo ,hapa tunaangalia vijana wa kitanzania lazima wawe na fikira kubwa zaidi kuwa wanaposoma lazima wakatumie taaluma zao kupambana na mazingira ,ili kubadili mazingira hayo kuwa fursa na ajira pindi watakapo maliza masomo yao na kwenda uwandani kufanya shughuli zao.
Pia maslahi ya wafanyakazi hasa walimu,ambao ndio wanatoa taaluma hii,hili ni kundi kubwa la wataalam wanaotegemewa kutoa elimu nchini kwaiyo ni vyema wakaangaliwa kwa jicho la pili ili wafanya vizuri zaidi kwa vile wao ndio kitovu cha shughuli hii na ndio wanakutana na changamoto za kutosha kutoka kwenye jamii na wanafunzi.
Na mitihani ya kumaliza elimu zao pia iwe ya kipimo sahihi,kwa mfano mitihani ya darasa la Saba ya Sasa hivi ni kuchagua tu mpaka masomo ya hisabati ,hii haimjengei mwanafunzi kumbukumbu ya kudumu na kuwa na uwezo wa kufikiri na kufanya maamuzi.
Utatuzi wa changamoto hizi ndio chanzo cha mafanikio serikali ni vyema ijikite katika kuhakikisha inaboresha miundo mbinu ya shuleni kwa kujenga madarasa ili kupunguza msongamano wa wanafunzi darasani ili waweze kupata masomo kwa ufasaha .
Pia serikali ni vyema kuboresha maisha ya walimu ili wawe na moyo wa kufanya kazi kwa jitihada ili kuongeza ufaulu shuleni.
Pia ni vyema serikali kupitia upya mfumo wa elimu kuanzia darasa la Kwanza la chuo kikuu katika ngazi zote, ambapo ngazi ya msingi, sekondari, VYUO vya kati na vyuo vikuu ihakikishe vyumba vya kutosha vya madarasa, matundu ya vyoo na nyumba za walimu na kuhakika, na kuhakikisha kuwa na zana bora za Kufundishia na kujifunzia kwa Kama vile vitabu na chai na pia yote haya yanakamilika endapo serikali itahakikisha inaboresha mtaala utamwandaa mwanafunzi kuwa mtu wa kwenda kupambana na maisha baada ya kupata elimu ambayo ni bor.
Mwisho ili tufanikiwe katika mambo yote hayo tujikomboe kutoka apa tulipo hatuna budi kuzingatia hivo vipaumbele katika mfumo wa wetu wa elimu.

Upvote
0