SoC04 Ukombozi wa kiuchumi wa Tanzania upo mikononi mwetu

SoC04 Ukombozi wa kiuchumi wa Tanzania upo mikononi mwetu

Tanzania Tuitakayo competition threads

Kidagaa kimemwozea

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2018
Posts
3,680
Reaction score
6,554
Zaidi ya miaka sitini pamoja na juhudi mbalimbali zilizofanyika bado uchumi wetu niwakujikongoja huku bado tukipambana na maadui wale wale aliowataja mwalimu Nyerere, Umaskini, ujinga na maradhi. Bado kungali na wimbi la umaskini miongoni mwa watanzania huku tukiachwa nyuma kimaendeleo na baadhi ya nchi zilizopata Uhuru baada yetu au miaka michache kabla au baada yetu kama vile China na Kenya.

Tulipofikia bado tunayo safari ndefu kufikia maendeleo yakweli ya kiuchumi na kuwa na dola yenye nguvu kiuchumi. Ndiposa katika makala hii nitaeleza miakakati maridhawa ambayo inaweza kutusukuma zaidi katika mapinduzi ya kiuchumi tunayohitaji.

Mosi, Nilazima tuhakikishe tunakomesha ubadilifu wa namna yeyote ule wa fedha za umma na miradi ya maendeleo; Uzalendo wa kiwango cha juu unahitajika katika hili, kwa wasimamizi wenyewe wa miradi ya maendeleo na fedha za umma kuhakikisha wanajizuia kufanya ubadilifu na pia kuwepo na chombo chenye makali Cha kusimamia mienendo ya viongozi hasa wale wasiozingatia maadili ya utumishi wa umma. na kufuatilia mitiririko yote ya fedha za maendeleo. Tukishaziba mianya hiyo tunaweza kuenda mkakati wapili kama ifuatavyo

Pili, Kuongeza saa za uzalishaji kuanzia ngazi ya kaya hadi taifa kwa weledi; Hapa tutazingatia kuongeza saa za kufanya kazi katika ngazi ya kaya , Taasisi za umma na binafsi lengo kuu ikiwa nikuongeza uzalishaji wenye tija. Kwamfano kiwanda kinachofanywa kazi kwa saa 10 kitataikiwa kuongeza saa 3 za ziada, ofisi ya umma iliyokuwa inafanya kazi kwa saa 8 utatakiwa kuongeza walau saa 3 za ziada lengo kuu ikiwa nikuongeza uzalishaji.

Vilevile katika ngazi za kaya na mtu mmoja mmoja atatakiwa kuongeza muda wake wa kufanya kazi , jambo hili likifanyika kwa moyo na kila mtanzania akijituma kuanzia shinani hadi ngazi ya Taifa , Taifa hili litapiga hatua baada ya mkakati huo lazima tufanye makakati watatu kama ifuatavyo,

Tatu, Kubana matumizi katika ngazi ya familia hadi ngazi ya taifa; Chomvya chomvya humaliza buyu la asali, kama nchi tukitaka kufanya mapinduzi ya kiuchumi nilazima tuhakikishe tunaweza kubana matumizi kwa kiwango cha juu kuanzia ngazi ya familia mpaka taifa.

Hii nipamoja na kusitisha huduma na matumizi ya ziada (yale yasiyokuwa ya lazima) kwa mtu mmoja mmoja na taasisi za umma kwamfano misafara ya viongozi kuwa ya wastani, kuondoa sherehe zizizokuwa na umuhimu sana za kifamilia hata taifa, kuzingatia zaidi usafiri wa bei nafuu miongoni mwa mambo mengine bila kuathiri utendaji. Baada hayo tunaweza kuongeza mikakati ifuatayo

Nne, Kutafuta watu wenye akili na maarifa ya ubunifu ndani na nje ya nchi nakuwapa nafasi; Kama marekani wanavyofanya kuwapa uraia wageni wanaoona wanaweza kutoa mchango wao katika kuinua uchumi wa Marekani hata sisi tunaweza kuiga kwa kuwapa nafasi watu wenye maarifa na ubunifu mkubwa kutoka nje ya nchi kuongoza taasisi zetu na wakatuletea mafanikio makubwa.

Pia, kwa wabunifu wa ndani wanaweza kupewa nafasi na kufanya vizuri pia. Hapa nashauri kiundwe chombo mahususi cha kijasusi kwaajili ya kutanabaisha watu hawa

Tano, Uwekezaji kwenye sekta ya kilimo cha kisasa utiliwe maanani; Kwa miaka mingi pamoja na kuwa na sera ya kilimo kwanza na kilimo kuwa ni uti wa mgongo wa Tanzania bado sekta ya kilimo haijawa na tija kama inavyotatikana, bado wakulima wengi wanalima na kufuga kilimo cha kizamani ambacho kimsingi hakina tija tena. Hiki nipamoja na kilimo cha kutegemea mvua pamoja na kilimo cha jembe la mkono.

Nashauri tungeweka mkazo katika kilimo cha umwagiliaji kutokana na Tanzania kuzungukwa na vyanzo vingi vya maji na kwa mikoa yenye ukame tunaweza kutengeneza malambo makubwa kwaajili ya kuvuna maji ya mvua ambayo yatatumika katika umwagiliaji wa mazao kipindi cha ukame.

Ili kufanikisha hilo itabidi kuongeza bajeti kubwa na toshelevu katika sekta ya kilimo ambayo itashughulikia kuwawezesha wakulima kulima kilimo cha kisasa na kutengeneza pamoja na kuboresha miundombinu ya umwagiliaji.

Aidha mafunzo na elimu ya kilimo nimuhimu kutolewa katika ngazi zote za elimu kwa vitendo ili kuwaandaa wanafunzi kuwa wakulima hodari na wakisasa pindi watakapo hitimu masomo yao. Vile vile kutunisha bajeti ya kilimo kunaweza kusaidia katika kutafuta wataalamu wa masuala ya kilimo wa kimataifa katika nchi zilizofanikiwa katika kilimo cha kisasa ili kuwashauri wakulima wetu.

Pamoja na hayo mchakato wa kubadilishana wataalamu na mataifa mabalimbali katika sekta mbalimbali nchini Kama vile elimu ya juu unaweza kutusaidia kutukomboa kiuchumi kwani wataalamu wa nje wanaweza kutuletea maarifa mapya ambayo tunaweza kuyatumia katika mapinduzi ya kiuchumi.

Mpango huo unaweza kuhusisha kuomba wahadhiri kutoka vyuo vikubwa duniani kuja kutoa masomo katik vyuo vyetu. Hayo tu nibaadhi ya mambo tunayoweza kuanza nayo katika mchakato wa kukua zaidi kiuchumi yapo mambo mengine Kama vile kupiga vita rushwa, utawala bora, na kuendelea kudumisha uhuru wa vyombo vya habari.
 
Upvote 0
Back
Top Bottom