Moaz
Member
- Apr 6, 2018
- 88
- 127
Hivi karibuni kumekuwa na hamasa kubwa miongoni mwa vijana wa Gen Z katika kuibua changamoto mbalimbali zinazowakabili ikiwemo maisha magumu,uhaba wa ajira,ukiukwaji wa haki za kibinadamu,utekaji n.k.
Na njia ambazo zimekuwa ni maarufu zaidi katika kuwasilisha maoni yetu kwa Serikali ni njia ya Maandamano ambayo ima yameratibiwa na Wanasiasa au wanaharakati na njia ya kuzungumza au kukemea kupitia mitandao ya kijamii kama Vile X(Twitter), Instagram, Facebook, Clubhouse, JamiiForum n.k.
Njia hizi zimekuwa ndio tegemeo haswa kwa vijana wa Gen Z kuweza kuwasilisha maoni pamoja na kushinikiza kuleta maendeleo ambayo yanaonekana kutotimizwa na Serikali.
Gen Z kwa mtazamo wangu ndicho kizazi ambacho kina kila sababu ya kutufikisha kwenye nchi ya Ahadi nchi ambayo Waasisi wetu wamekuwa wakiiota. Kufikia mafanikio hayo Gen Z wanapaswa kuja na mbinu ambazo zitakuwa madhubuti kwa ajili ya mapambano haya makubwa ya kihistoria.
Kwa kuwa Njia za maandamano hazikuwahi kuja na utatuzi wa muda mrefu wa maswala mbalimbali ya kijamii hivo kama Gen Z tutahitajika tuje na njia ambazo tutazitumia katika harakati zetu za ukombozi wa taifa letu.
Katika zama hizi za Gen Z moja ya jambo tunajivunia ni uwepo wa Technology haswa hii ya habari ambayo imeweza kuwezesha kila mwananchi kupitia simu yake anaweza kutoa maoni au kuzungumza chochote ambacho anaona ni sahihi kwake.
Jambo hili linaweza kuwa ni sahihi ila ni jambo ambalo halina hiyo effects ambayo wengi wetu tunaifikiria. Kwa kuwa Kutoa maoni au kuandika taarifa pasina kuwa na Elimu nayo ni hatari sio tu kwa mtoa maoni ni hatari hata kwa jamii itakayo yapokea hayo maoni.
Ni muda sasa Gen Z kuja na njia ambazo zitakuwa ni suluhu ya matatizo ya jamii yetu ya sasa na ya hapo baadae. Tunafahamu kuwa Gen Z ni kizazi ambacho kinajivunia Technology ya hali ya juu kuliko zama zote. Technology ambayo imefanya Dunia iweze kuwa kama kijiji hivo kupelekea matatizo makubwa ingawa wengi wanaamini Utandawazi ni chanzo cha maendeleo.
Mtazamo wangu Utandawazi ni kama kisu ambacho kinaweza kuwa na manufaa kwa jamii au kuwa tatizo kwa jamii kivipi? ni kuwa matumizi ya utandawazi pasina kuwa na elimu nao hutengeneza Mawazo yasio na hekima ambayo ni hatari katika jamii na Taifa kwa ujumla.
Tukiangalia ni jinsi gani GenZ wamekuwa expose na utandawazi tunapata picha kuwa kabla ya harakati zozote za ukombozi inatakiwa Gen Z watambue wapi tumetoka na wapi tunataka kwenda hili jambo la msingi sana kabla ya harakati zozote za ukombozi.
Je ni mambo gani ambayo Gen Z tunapaswa kuyatambua kwanza kabla ya harakati zozote?
Kwa mtazamo wangu Jambo la muhimu kabisa ambalo Gen Z wanapaswa kulitambua ni Utambuzi wa Ukweli na Uhalisia wa mambo mbalimbali.
Kuna mambo mengi yanaendelea katika jamii kuanzia kwenye Siasa, Uchumi, Afya , Technology n.k ukweli unahitajika katika kuyaendea haya mambo. Ukweli ni nini? Ukweli ni elimu na maarifa sahihi kuhusu mambo mbalimbali yanayotuzunguka katika jamii na Taifa kwa ujumla.
Katika zama zilizopita watawala waliweza kuuficha Ukweli kwa kila aina ya Propaganda kiasi kwamba mpaka sasa ni ngumu kuweza kuona Ukweli na uhalisia wa mambo. Gen Z ndicho kizazi ambacho kwa sasa kinaathirika na hizo Propaganda hivo ni jukumu la Gen Z kuweza kutafuta Ukweli wa mambo ili kuweza kujinusuru kama Taifa na jamii yetu kwa ujumla.
Binaadamu wote tuna haki ya kuujua ukweli ila wachache ndio wako tayari kuutafuta ukweli kwa kuwa ukweli siku zote unatisha na ni kama kisu kikali hivo watu wengi wanahofia ima kwa hofu ambazo wametengenezewa au kwa Mazoea tu ya kutokuwa watafuta ukweli wa mambo ili kuweza kuwa sehemu salama.
Kutafuta ukweli haswa kwenye swala zima la Siasa na Uchumi ambazo ndizo sehemu zinazobeba Taifa kwa ujumla ndipo nafikiri vijana wa Gen Z tunatakiwa tuanzie hapo.
Swali: Ni ipi Hali ya siasa na uchumi wetu ambazo ndizo sehemu muhimu katika ustawi wa Taifa letu ukoje?
Mtazamo wangu ni kuwa Siasa zetu na uchumi wetu zimegubikwa na mambo mengi ambayo hayana uhalisia. Labda naweza nikawa sina maono hayo ila kufikia mpaka sasa miaka 60 ya uhuru Tanzania tulipo sipo tulipo paswa kuwepo. Kuna mambo mengi yanatokea katika jamii lakini kwa kuwa hatuna jicho la kuona ukweli wa mambo tumekuwa ni watu wa kuyatazama na kushindwa kutambua kama ni uongo mtupu na propaganda za viongozi.
Mara kwa mara najiuliza ni kweli viongozi wanafanya kwa makusudi au nao pia hawatambui ukweli wa mambo. Swali hilo nimekosa majibu bali nilichugundua kuwa Taifa letu linaendesha siasa za uongo kwa kuwa jamii kubwa ya watanzania hatuna maarifa ya kuweza kuutambua huo uongo.
Na kwa viongozi Hii inakuwa faida kwao hivo wanafanya mambo ambayo kimsingi ni propaganda tu kwa kuwa wanatambua wananchi hawana uwezo na uthubutu wa kutambua na kutafuta ukweli wa mambo ukoje.
Nikianzia kwenye Siasa moja ya sehemu muhimu katika kila taifa duniani ila kila mtanzania anafahamu sehemu hii ndio sehemu iliyojaza wajinga wengi ambao hawana uelewa wa mambo mbalimbali kwa kuwa wametanguliza Tamaa za kutaka kufanikiwa kwanza wao na familia zao. Ni ngumu sana ukute Kiongozi wa kitanzania anajiuliza swali la Watanufaikaje wananchi hawa walionichagua?
Kiongozi sio mtatuzi wa Matatizo hapana kiongozi ni mtu ambaye anaongoza watu wake katika utatuzi wa matatizo mbalimbali yanayo wakabili katika jamii yake kwa kuwa tayari ana rasilimali watu na mamlaka pia ni kazi yeye na watu wake kuja na mawazo ya utatuzi wa matatizo yanayowakabili kwa kusaidia na serikali.
Kila mtanzania anaona na anajua ni jinsi gani viongozi wa Taifa letu wanavofanya kazi zao kwa udanganyifu ambao umefichwa kwenye katiba na sheria ambao pia hiyo katiba wanaitumia vibaya ila wananchi hawataki kuona ukweli kabisa sijajua labda kwa vile asilimia kubwa ya wananchi hatuna maarifa au jicho la kuona uhalisia na ukweli.
Viongozi wanakuja kwa wananchi nyakati za uchaguzi kama hivi na akija anapiga propaganda zake ili atumie nguvu ya wananchi ambao hawana uelewa na maarifa ya mambo. Then anarudi kama kawaida na huu ndio mzunguko na kila mwananchi anajua ila hatuna uthubutu wa kusema kwa kuwa hatujui kama hilo jambo ni Kweli au laa.
Taifa letu limejaa viongozi wenye tamaa ya kufanikiwa wao na sio wananchi, nafahamu duniani kote viongozi wako hivo sio viongozi tu kila mwanadamu ana hiyo nafsi ya ubinafsi ila utofauti ambao uliopo ni kuwa viongozi wa mataifa yaliyo endelea wao wanafanya biashara ya siasa kwa kuwapa huduma nzuri wananchi na wao ndio wanaponufaika katika kutoa hizo huduma kwa kuwa The more you serve the more you earn Simple Rule. Ila kwa bara letu la Afrika iko tofauti huku The more you are not serve the more you earn.
Hivo ndio maana tunasikia ufisadi mara kwa mara mpaka sasa imekuwa kawaida katika Taifa letu kiasi kwamba kila Mwananchi anaamini ukiwa serikalini lazima upige hizo pesa kwa kuwa usipopiga utakuwa hujafanya kazi ya kiongozi.
Huu ukweli kama Gen Z tunapaswa kuukubali na kuutafutia suluhu ya kudumu kama tutakaa na kuuishia kuandamana tu pasina kuwa na maarifa sahihi ya kuweza kuona mabaya zaidi ya haya tutaishia kuwa wananchi masikini katika karne hii na kuweza kutumika kwenye hicho wanachokiita Democracy na ukweli kwamba hatujawahi kuwa na hiyo Real democracy kwasababu ni hatari kwa ustawi wao.
Ni aibu kwa Viongozi na Taifa kwa ujumla kuwa na idadi kubwa ya Umasikini nchini achana na hizo taarifa zao za kupikwa kuwa pato la mtanzania limepanda ukweli kwamba hizo taarifa ni asilimia 100 zinapikwa na watawala ili kuweza kuzitumia kumanipulate wananchi lakini sio kweli.
Maana hivo vyombo vya habari vinamilikiwa na wao na wao ndio wanapanga nini waseme na nini wasiseme na ndio maana taarifa ambazo utazisikia ni zile zile kila siku Kuisifu Serikali, vifo , mafuriko, connection,matamasha ya starehe, matangazo ya pombe,mipira n.k lakini hutosikia ukweli wa mambo hata hivo taarifa nyingi ni mitazamo yao kwa upande wao wanavoiona taarifa then ndicho wanachokuja kukitema na kuilisha jamii ambayo haina maarifa ya kuweza kutambua ukweli.
Nini kitatokea hapo?
Akili ya Mwanadamu inakuwa kile kinacholishwa. Akili haina muda wa kuujua ukweli kama ukweli haupo Akili basi itajichanganya na ujinga baada ya hapo ni hatari kwenda mbele.
Sasa ni muda wa Gen Z kuuweka ukweli wa mambo katika uelewa wa kila mtanzania tuna technology ambayo imekuwa kama ndio symbol yetu na silaha yetu kubwa katika mapambano yetu. Ni muda sasa wa Gen Z kutoka huko walikotupeleka na wanapotupeleka katika mambo ya betting, unywaji wa pombe, starehe za kila aina pamoja na kutuweka busy kwenye mitandao ya kijamii kwa kutulisha ujinga kama vile maconnection na mambo mengi tu ambayo hana faida katika Taifa letu. Kwanza tufanye wajibu wetu kama vijana kwa kupambania Taifa bora lenye wananchi ambao wana maisha bora.Then hayo ya starehe yatafuata.
Swali: Je Gen Z tunaweza kulifanikisha hili?
Nina imani Gen Z ndio wakombozi wa Taifa hili kama tutataka na tukiwa tayari kuibeba dhamana hiyo japokuwa kuna changamoto moja kubwa sana katika harakati hizi. Tuna tatizo kubwa la kutokuwa na Umoja. Leo Gen Z kila moja wetu utakuta ana account ya social network na yupo active akiamini yupo connected na ulimwengu na hivo akili inatengeneza uongo wa kuamini hicho anachokiamini.
Ukweli ni kwamba social network zinaweza zikawa ndio silaha yetu ila social network imeshatuharibu kiasi kwamba sahv imekuwa ni silaha ambayo inatudhuru wala sio kutusaidia katika maendeleo yetu kama Taifa. Kwanini nasema hivo?.
Social network ni kweli zinatukusanya watu mbalimbali na tunaweza kushare habari tofautitofauti zinazotukabili katika jamii hili linaonekana kama jambo zuri ila ukweli ni kwamba hili ni jambo baya zaidi kwa kuwa hili ndilo linasababisha watu kuwa disconnected.
Maana ya kuwa Connected ni kuwa katika Network sahihi yenye lengo moja.Vijana wengi tupo kwenye Social network but hatupo Connected kabisa kwa kuwa wengi ambao tunao na tunashare nao habari sio ambao tuna mtazamo inayoshabiiana ndio manaa ukiingia kwenye social network ni Confusion kwenda mbele kila mtu ana mawazo yake na kila mtu anapost anachojisikia yaani ni sehemu hatari zaidi kuwepo kama utaweza kuona ukweli. Social network ndizo zinatumika kutugawa Gen Z.
Ila sasa ni muda wa sisi kutumia Social network kutuunganisha kuwa kitu kimoja. Kwa kuwa naamini silaha inayotumika kukudhuru pia ndio silaha inaweza kukulinda na madhara.
Hakuna jambo ambalo linawatisha watawala wa ndani na nje ya nchi kama umoja na hili swala ni hatari zaidi kuliko tunavofikiria. Tunapaswa Gen Z kuwana na community zetu ambazo tunafahamu fika zinashabiana mawazo hii itatengeneza strong community kwa kuwa watu wanaongea lugha ambayo wanaelewana.
Mfano watu waafya wawe na social network yao, walimu, madereva, wafanyabishara, wanafunzi n.k kwanini tuwe na hizo community. Taasisi nyingi ambazo wananchi haswa hao wafanyakazi wapo hazipo kwa ajili ya kutetea maslahi yao Taasisi nyingi zimeweka kuzuia wao kuwa kitu kimoja kwa kuwa kama wafanyakazi wataungana kuanzia kwenye sehemu zao za kazi ni hatari kwao kisiasa na kiuchumi hivo zimetengenezwa hizo taasisi kwa ajili ya kuwazuia kuwa kitu kimoja.
Nina imani wafanyakazi haswa wanahudumia jamii ndio nguvu iliyofurugwa na watawala ili waweze kucontrol na kubaki kwenye nguvu.Gen Z tunatakiwa tuunganishe hawa wananchi/wafanyakazi ili tuweze kutengeneza umoja wenye nguvu.
Nafahamu fika katika Nchi yetu swala la umoja ni ngumu na hiyo hi kutokana na umasikini ambao utatufanya ni rahisi wengi wetu kununulika na kutumika na watawala kama toilet paper.Je nini tuunganike? Tunafahamu moja ya sababu kuu wafanyakazi wengi wamo humo ni uoga na hiyo ndio sababu wanashindwa kuzungumza kwa kuwa wanahofia kupoteza ajira zao.
Ajira ambazo wanatumia kutunzia familia zao Tanzania bado jamii nyingi zipo kwenye extended family mtu mmoja anakuwa na Impact kubwa kwenye familia yake hii inawafanya wafanyakazi wengi wawe kimya na kushindwa kuongea ukweli ingawa wanafahamu fika kuwa sio sahihi na wananguvu ila hajui cha kufanya.
Katika zama za Technology hili tatizo linaweza kutatuliwa kwa kuwa na Online community ambazo mtu hatotumia jina lake asili japokuwa kuna changamoto itakuwepo kwenye kumuhakiki lakini nina imani ipo njia ya kutatua hili. Mfano mzuri ni JamiiForums humu wananchi wanazungumza mambo mbalimbali katika majukwaa husika ila sio kwa watu husika namaanisha still bado kuna kitu kinakosekana katika kuwaunganisha wananchi.
Kwa maana yangu ni kuwa tunapaswa kuwa na community za wafanyakazi ambao wanafanya kazi katika sekta moja kwa kuwa kuunganika kwa wafanyikazi hawa wataweza kuongea ukweli uliopo ndani ya mazingira yao nini mazuri na nini mabaya na njia ya kuweza kutatua hizo changamoto pasina mtu kutambulika kiasi akarisk kazi yake hivo itakuwa ni kazi sasa ya kuchukua mawazo ya kila community na kuyatumia katika kutengeneza na kuleta maendeleo katika jamii.
Online Community kwa mtazamo wangu ndio mwanzo wa kutengeneza umoja ambao watawala wameuharibu kwa kutengeneza taasisi zao na kuwapa uoga so Technology ipo kwa ajili ya kuwatoa kwenye kifungo hicho ni kazi ya Gen Z kutengeneza hizo community kwa ajili ya kutengeneza umoja.
Taasisi nyingi ni propaganda tu hazipo katika hicho wanachohubiri so Gen Z ni muda wetu kuleta community za kweli ambazo watu watapeana maarifa ya kuona ukweli ambao na kuusema kwa jamii ambao ni muda sasa ulifichwa na kuelezea uongo ambao wanauona lakni walishindwa kuelezea kwa kuhofia usalama wao.
Kwa Mtazamo wangu ninaimani kama Gen Z tutaanza na hizi hatua mbili ambazo kwanza ni Kutafuta Ukweli ambao ni Maarifa sahihi na Kuungana katika kupeana hayo Maarifa kwa hakika tutakuwa tupo katika njia ya kuitafuta Nchi ya ahadi. Hivo wito wangu kwa Gen Z wenzangu ni muda sasa wa kutafuta maarifa katika kila jambo ambalo linatuhusu najua kuna Swali la ni vp tunaweza kutafuta maarifa ya kweli?
Katika Zama zetu ni utayari na uthubutu ndio chanzo cha kupata maarifa yeyeto unayo yataka Japokuwa katika zama zetu hizi kuna wingi wa taarifa kiasi kwamba kama hutojua ni taarifa gani inaweza kuwa na faida kwako na kukuletea maarifa inaweza ikawa changamoto kwasababu hata huku kwenye maarifa pia pamekuwa manipulated kwa mtazamo wangu nafahamu kama GenZ kam tutakuwa na clear goals tutaweza kujua ni maarifa gani yatatufaa katika safari yetu ya kwenda nchi ya ahadi.
Hivo itakuwa vyema kwa vijana ambao wana maarifa ambayo wanaona kuwa yanamanufaa aweze kutoa maarifa hayo katika community husika ili kuwafungua na wengine. Natamani kuona Gen Z inakuwa jamii Bora zaidi kutokea sio kwa ajili ya kupeana Odds na Connection mitandao bali kupeana maarifa ya kuweza kutambua ukweli katika mazingira yetu.
Utambuzi wetu wa Ukweli na Umoja wetu madhubuti ndio msingi wa kuifikia Nchi ya ahadi. Kwahiyo ni wito wangu kwa Gen Z tuamke Taifa linatuhitaji mno zaidi ya tunavofikiria