Ukomo wa miaka ya kusoma uzamili/ masters katika vyuo huria

Ukomo wa miaka ya kusoma uzamili/ masters katika vyuo huria

GHabari zenu,k

Naomba mnijuze ukomo wa kusoma masters katika vyuo huria.

Nauliza maana ni miaka karibu sita sasa shemeji yenu anasoma tu hiyo elimu. Vikwazo vimekuwa vingi mno masters haiishi mpaka namuonea huruma.
Hujaeleza kwa kina. Ila ina wezekana kuna kipindi aliomba kuahirisha masomo. Je anasoma program gani hapo?
 
Kama anasoma UDSM inawezekana kupiga miaka hata 9. Wale jamaa ni wadzwanzi balaa hasa kama undergraduate hukusoma pale. Jamaa zangu wa ofisini wana huu mwaka wa 8, mwingine ameamua kuachana nayo kabisa.
Ni shida mkuu hata hapo Open kwenye Masters by Thesis or research only watu wanasoma mpaka miaka 6 Masters na wengine wanaamua kuacha kabisa.
 
Ni shida mkuu hata hapo Open kwenye Masters by Thesis or research only watu wanasoma mpaka miaka 6 Masters na wengine wanaamua kuacha kabisa.
Siku hizi watu wanakimbilia masters za kuokota kutoka vyuo kama IFM, IAA, CBE, Udom, Sauti nk. Vyuo vingi hapo wana masters za online unasoma mwaka mmoja umemaliza na kupewa cheti kimenyooka na GPA yako ya 32..

View: https://youtu.be/hcLffSjBNlU?si=gIF10nvojotQ7uFL
 
Maybe research ndo inamchelewesha
Maana Research report za post graduate sio pw....
 
Kuna wengi wamedrop kwasababu ya tabia za hovyo za baadhi ya wahadhiri, wanawake wengi huombwa visivyoombeka
Hii ni kweli kabisa! Wahadhiri wanatumia kigezo cha "wote ni watu wazima, wanaosoma na wanaosomesha"

Na mtu hata haogopi kwamba huyu ni mke wa mtu...

Kweli inasikitisha!
 
Kama anasoma UDSM inawezekana kupiga miaka hata 9. Wale jamaa ni wadzwanzi balaa hasa kama undergraduate hukusoma pale. Jamaa zangu wa ofisini wana huu mwaka wa 8, mwingine ameamua kuachana nayo kabisa.
Kweli kabisa! Kuna jamaa yangu mmoja yeye kwao pesa ipo!

Alisoma hapo wakamletea uduwanzi akaacha... Alikuwa anaandaliwa kurithishwa mamlaka aongoze makampuni na mabiashara mengine.

Ila mpaka leo yupo vizuri maradufu, akili alikuwa nayo ila hataki kusikia kuhusu kusoma tena.
 
Back
Top Bottom