Insabhunsa Gusa
Senior Member
- May 13, 2011
- 109
- 88
Wana JF,
Kama Raisi, Waziri, Mbunge nk ni watumishi wa umma. Kwa nini rasimu ya KATIBA mpya haijatamka umri wa ukomo kugombea nyadhifa hizo, ilhali imetamka umri kianzio wa miaka 40 kwa uraisi.
Nijuavyo, umri wa ukomo wa utumishi wa umma ni miaka 55 kwa hiari na miaka 60 kwa mujibu wa sheria. Nilidhani Raisi kama mtumishi wa umma, hatakiwi kuwa madarakani akiwa na umri zaidi ya miaka 60!!! Napendekeza, umri wa ukomo kugombea Uraisi, ubunge, uwaziri, ukatibu mkuu nk nk nk uwe miaka 50, ili atumikiapo vipindi/awamu mbili awe na miaka 60, tayari kwa KUSTAAFU!!!!!! Yasije yakatukuta ya BABU Mugabe, tusilaumu tu pengine Katiba ya Zimbabwe inaruhusu umri wowote.