SoC04 Ukomo wa Uongozi chachu ya ajira

SoC04 Ukomo wa Uongozi chachu ya ajira

Tanzania Tuitakayo competition threads

dinoza

Member
Joined
Jun 22, 2024
Posts
8
Reaction score
5
Uchaguzi wa raisi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania,huchaguliwa kila baada ya miaka mitano baada ya miaka hiyo hulazimika tena kurudi kwa wananchi na kuomba kura tena,mara nyingi maraisi wa Tanzania huongoza kwa mihula 2,ambayo ni sawa na miaka 10.mfano halisi ni maraisi waliopita waliweza kuongoza nchi kwa miaka 10 mfululizo na kuachia ngazi.

KWANINI AJIRA IMEKUWA CHANGAMOTO
Ajira imekua changamoto kutokana na kwamba viongozi wengi wanakaa madarakani kwa muda mrefu sana kitu ambacho husababisha ajira kutokupatikana,kwa kawaida raisi hukaa madarakani kwa kipindi cha miaka 5 hadi 10 kisha hupisha na kuanchia ngazi,lakini kuna viongozi wanakaa madarakani kwa kipindi cha miaka 30 mpaka 40 yupo serikalini anabadilisha nyazifa tofauti tofauti,kitu ambacho sio sawa,kama raisi anakaa madarakani kwa kipindi cha miaka 5 mpaka 10 kwa nini sasa na hawa viongozi wasifanye kama anavyo fanya raisi,

MTU AKIAJIRIWA SERIKALINI KATIKA NYAZIFA YEYOTE ILE AITUMIKIE KWA KIPINDI KISICHOZIDI MIAKA KUMI.
Tunahitaji kila mwananchi mwenye sifa na vigezo vya kuwa kiongozi basi aweze kupewa nafasi na atakapo maliza muda wake basi aachie ngazi.nashangaa na inasikitisha kiongozi kua madarakani kwa kipindi kirefu miaka 30 mtu yupo uongozini kiasi kwamba serikali anaifanya kama familia yake,tusikilizane kwa makini hatutaweza kufanya mabadiliko na maendeleo kwa nchi yetu kama viongozi wale wale wapo madarakani kwa mda mrefu na kufanya wanayojua wawa

KIONGOZI KUA NA AINA MBILI ZA KAZI KWA WAKATI MMOJA
kunaviongozi wengine wana kua na nyazifa tofauti tofauti kwa wakati mmoja,unakuta kiongozi ni waziri,mbunge,yani nafasi mbili kwa wakati mmoja kitu ambacho sio sawa kitu kinachopelekea kua na ufinyu wa aajira.

NINI KIFANYIKE ILI KUPUNGUZA UKOSEFU WA AJIRA

*Kupunguzwa kwa muda wa viongozi madarakani,mfano kiongozi atakae kua serikalini afanye kazi kwa kipindi kisichozidi miaka 10 kisha alipwe mafao yake na hatoweza kuajiliwa tena serikalini baada ya mda wake kuisha.

*kiongozi kuwa na aina moja ya kazi kila baada ya miaka mitano kwa muda usiopungua miaka kumi.
viongozi wasing'ang'anie madarakani kwa muda mrefu unakuta kiongozi alisha kuwa mbuge,baada ya miaka 5 anakua waziri wa kilimo,huyohuyo baada ya miaka 5 tena anakua waziri wa madini,baada ya miaka 5 tena huyohuyo anakua waziri wa fedha,mi nauliza tu kwa nia njema kwani hakuna wananchi wengine wenye sifa hizo za kuongoza kiasi cha kiongozi kuongoza miaka takribani 40
 
Upvote 2
Back
Top Bottom