Ukomo wa Urais, laana inayomwandama Nkamia

Kinoamiguu

JF-Expert Member
Joined
Nov 29, 2018
Posts
11,936
Reaction score
15,196
Hongereni Wanasimba kwa kukataa huyu mnafiki. Bwana Juma Nkamia ameangukia pua puu katika uchaguzi wa Simba hapo jana.

Nkamia ni mtu mwenye majivuno mengi.

Ni yeye aliyewahi kuja na hoja ya kutaka JPM aongezewe muda wa kututawala.

Ni yeye huyu aliyewahi kuwaita Wapinzani Mbwa alisema haongei na mbwa anaongea na mwenye mbwa.

Sasa siyo mbunge, hana cha kufanya anataka akagange njaa kwenye mpira.

Wanasimba wakamuangusha puu.

Hongereni kumwangusha mjivuni huyu Juma Nkamia.
 
hili li Mnkamia ni jitu la majungu tu hata ukitafakali michango yake bungeni ilikuwa ni majungu tupu kuomba rais anayegasi watu aongezewe muda lilikuwa linategea uteuzi baada ya kupuuzwa likanyamaza halikujua kumbe hadi jimboni likawa limeudhi watu.
 
Juma Nkamia ametumia hakiyake ya Uhuru wa kuongea si vizuri kumshtumu kwakua mmetofautiana ki mtazamo. Democracy inataka wengi wapewe wachache wasikilizwe. Msichukiane kwakua mmetofautiana.
 
Haki gani ya kuzungumza mambo ambayo katiba hairuhusu...!
Na kwenye mchakato wa kutafuta katiba mpya hakuchangia chochote kile.
Mtu anazungumza jambo lililo nje ya taratibu za katiba ya nchi ndo anaambiwa ana haki ya kuzungumza...!
Tena analizungumza Bungeni bila kutumwa na wananchi wake ambao kwenye Tume ya Katiba Mpya hawakuhitaji nyongeza ya miaka na vipindi vya uraisi.
Ati raisi aongezewe kipindi kimoja na kiwe cha miaka saba.
Ni kauli za kudharau maamuzi ya wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Maoni kama haya inabidi yatolewe kwenye tume ya katiba mpya na sio Bungeni.
Kauli kama hizi ni kujishushia heshima na kuishia kudharaulika mbele ya Jamii.
 
Juma Nkamia alikamia lakini hakuyanywa.
 
w
watu wa aina ya Nkamia hawatakiwi kuja kupewa uongozi tena maisha yao yote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…