Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Mbunge wa Ukonga ambaye pia ni Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Jerry Silaa amegawa majiko ya gesi ya kupikia kwa mama lishe jimboni kwake, ikiwa ni sehemu ya kampeni ya kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan za kuhamasisha jamii kutumia nishati safi ya kupikia.
Silaa alikuwa katika ziara jimboni humo ambapo amesema matumizi ya gesi ni salama na yanaokoa fedha nyingi pamoja na kutunza mazingira, ziara hii ikiwa ni muendelezo wa ziara yake jimboni humo aliyoianza Septemba 09, 2024.
Pia soma: Uzi Maalum wa Vibweka na Hekaheka za wanasiasa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Akiwa katika soko dogo la Pugu Mhe. Silaa alizungumza na Wafanyabiashara ya chakula ambapo aliwataka kutathmini matumizi ya mkaa na gesi.
"Ndugu zangu tumieni majiko haya ya gesi na mfanye tathmini ninyi wenyewe ni nishati ipi inayotumia gharama kubwa" amesema Silaa.
"Mimi natumia mkaa wa shilingi elf 7 hadi 8 kwa siku, ni gharama kubwa ambayo nikiuza chakula napata faida kidogo na wakati mwingine sipati kabisa, pia naumia na moshi wa kuni na mkaa ninaopikia," amesema Bi. Riziki Ramadhan Mkazi wa Pugu Kona.
Soma Pia:
- Naibu Waziri Nishati, Judith Kapinga asema "Nishati safi ya kupikia inabeba Ajenda ya Mazingira"
- Rais Samia Ameibeba Ajenda ya Nishati Safi ya Kupikia Kimataifa
"Mheshimiwa Mbunge, Mimi nimezaliwa mwaka 1949, na uzee huu hili jiko litanisaidia sana, nilikuwa natumia muda mwingi kutafuta kuni na mkaa, maisha yangu ni magumu sana, hajika mmenirahisishia maisha, nakushukuru wewe binafsi na Rais Samia kwa kutuletea maendeleo haya," amesema Khadija Kawegela.