Ukoo: Kumbe babu yako ndio wewe mwenyewe

Stoik

Member
Joined
Feb 14, 2021
Posts
27
Reaction score
67
UKOO!

Fikiria, Unaoa mwanamke ambaye tayari ana mtoto wa kike mkubwa. Kisha Baba yako anaoa mtoto wa mwanamke uliyemuoa.

Mtoto wa mke wako anakuwa Mama yako, baada ya Mtoto wa Mke wako kuwa Mama yako, Mke wako nae ambaye ni Mama wa Mama yako anakuwa Bibi yako!

Unashtuka Kumbe umeoa Bibi yako,Mwisho wa siku Mume wa Bibi yako anakuwa Babu yako, KUMBE BABU YAKO NI WEWE MWENYEWE!


Naamini kuna baadhi ya Koo / Familia, zina mvurugano flani ivi katika undugu. Kama mimi Shangazi yangu kaolewa na Babu Yangu!
 
Njaa ni kitu Cha hatari sana.
 
Kwamba unaoa mwanamke mwenye mtoto
Alafu yule mtoto anaolewa na baba yako
Mtoto wako anakua mama yako na mke wake anakua bibi yako

Hahaha kwa hiyo unakua umeoa bibi yako ina maana babu yako anakuwa wewe[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kama tu bibi yako ni mke wako sasa babu yako si atakuwa wewe
 
Wakati nasoma nimejing'ata akili mara 3 ndio nikaelewa
 
Sas mke wako utamuita Bibi au Mke na mtot wake utamuita mama au uo muunganiko wa ukoo hauelewek Dadek
 
Familia za ki Africa ziko disorganized huwezi amini unakuwa na uncle mwenye miaka sita
 
Mathematics [emoji28][emoji28]

Sent from my SM-G570F using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…