Pdidy
JF-Expert Member
- Nov 22, 2007
- 57,951
- 32,619
POLISI wa Kituo Kikuu cha Polisi Himo kilichopo Wilaya ya Moshi vijijini mwishoni mwa wiki walivamia na kuvuruga kikao kilichoandaliwa kwa lengo la maandalizi ya kumsimika Frank Marealle kuwa Mangi wa Wachaga wa Marangu.
Hatua ya polisi kuvuruga kikao hicho ilifuatia malalamiko kutoka Ofisi ya Kijiji cha Lyamrakana wilayani humo juu ya kuwapo hali ya uvunjifu wa amani endapo kikao hicho kingeruhusiwa kufanyika.
Taarifa ya Polisi Himo ya Juni 18 mwaka huu, kwenda kamati ya kumsimika Frank Marealle kuwa Mangi wa Marangu ilisema kuwa, pamoja na Serikali ya Kijiji cha Lyamrakana kutokuwa na mamlaka ya kuingilia taratibu za kijadi kwa kabila lolote, lakini polisi wamelazimika kuingilia hali hiyo ili kuleta amani.
Kimsingi ofisi hii haipaswi kuingilia utaratibu wa kijadi wa kabila lolote, lakini kwa vile malalamiko haya yameletwa kwetu na kutoa hadhari kwamba kunawezekana kabisa kutokea uvunjifu wa amani katika kikao hicho, tuna kila sababu ya kusitisha kikao hicho kama walinzi wa amani,ilisema barua hiyo.
Polisi walitahadharisha kuwa, kama walinzi wa amani hawatopenda kuona kunatokea uvunjifu wa amani na kushauri wanaoendesha kikao hicho kukaa na uongozi wa Serikali ya kijiji ili kutafuta ufumbuzi na kuhusisha pande zote.Hatua ya polisi kufuta kikao hicho, ilifuatia kusambazwa kwa barua za mialiko ya kuhudhuria kikao cha maandalizi ya kumsimika Frank Marealle kuwa Mangi wa wachagga wa Marangu kinyemela licha ya wanaukoo wa Chief Thomas Marealle II O.B.E, kutotambua harakati hizo kwa kuziita ni batili zenye lengo la kuyumbisha mila na desturi za ukoo huo.
Somo hapo juu linahusika,hudhuria kikao cha kamati ya Jumapili Juni 19, mwaka huu saa 7.00 mchana, kikao kitafanyika pale kwa Dk Wilfred Marealle saa 7.00 mchana, tafadhali zingitia muda, pia Mangi mtarajiwa Frank L Mlanga atakuwapo hivyo zingatia muda uliopangwa, inasema barua hiyo iliyosainiwa na Frank Nyaki kama mwenyekiti wa kamati.
Polisi walizuia kutoendelea kwa kikao hicho kilichokuwa kikifanyika nyumbani kwa Dk Wilfred Marealle katika Kijiji cha Lyamrakana Marangu kikao ambacho hata hivyo kinadaiwa kuandaliwa na watu wasiokuwa wana ukoo wa Marealle kutoka Kijiji cha Marangu Rauya zaidi ya kilometa saba kutoka Kijiji cha Lyamrakana.
Hivi karibuni baadhi ya wanafamilia wa Ukoo wa Chief Thomas Marealle II, walikutana na kutoa tamko la kutotambua harakati hizo za Frank kujitangaza kuwa Mangi wa Marangu na kumchagua Teddy Marealle kuwa mwenyekiti wa muda wa uko huo hadi Desemba 28, mwaka huu kitakapofanyika kikao cha wanafamilia wote walioko ndani na nje ya nchini.
Akitoa tamko mbele ya waandishi wa habari na wanafamilia hao Teddy alisema vikao hivyo ni batili na kwamba vina lengo la kuleta mgawanyiko ndani ya ukoo na kuongeza kuwa,taratibu za kumpata mangi wa Marangu kurithi nafasi ya Mangi Augustine Marealle mdogo wake na marehemu ,zitafuata taratibu za kimila na kitamaduni .
Mangi wa Marangu alikuwa ni Augustine Marealle ambaye alizaliwa Januari Mosi mwaka 1921 na alifariki dunia Novemba 26 mwaka 2006 wakati huo kaka yake, Chief Thomas Marealle II O.B.E, alikuwa mangi Mkuu wa wachagga wote enzi za utawala wa ki-chief. Tamko hilo la Ukoo wa Mangi Marealle lilitolewa mbele ya viongozi wa serikali ya Kijiji cha Lyamrakana wakiongozwa na Ofisa mtendaji wake, David Mkusu, mwenyekiti wa kitongoji cha Lyamrakana, Albert Mtui, mjumbe wa kamati ya ulinzi na usalama na mjumbe wa Halmashauri ya Kijiji, Daudi Lyamuya.
Wajumbe wengine wa Serikali ya Kijiji cha Lyamrakana waliofuatana na mwenyekiti wao ni Ernest Tilia Dresfori Kessy na Robson Kitali ambao waliunga mkono tamko la mwenyekiti wao la kutotambua uwapo wa makundi mawili katika ukoo wa Marealle.
Kwa upande Ofisa Mtendaji wa Kijiji hicho,alisema Serikali ya kijiji chake haitakubali kutokea kwa uvunjifu wa amani katika kijiji hicho kutokana na watu wachache kuendesha shughuli za siri bila kuhusisha Serikali ya kijiji.