Ukopaji fedha na jinsi unavyoua Urafiki

Ukimuomba laki anakupa elfu10 halafu anakwambia nimekupa tu sitokudai. Unajua kwenye maisha unatakiwa bandidu sometimes.
That's the way to go. Kuna mwingine yeye akiombwa mkopo anasema ana madeni bank na analipa 75% ya salary yake. Hakopi mtu yeyote yule. Unajua kuna marafiki wanakuja na shida genuine kabisa na unaguswa ila baadhi ya matukio yanapelekea mtu kujifunza ubandidu tu.
 
Bora umkopeshe mtu usiyemfahamu waweza mpeleka hata mahakamani, ila hawa tunaowajua inakula kwetu tuu!

Kuna rafiki yangu nilimkopesha pesa ndogo tuu toka july2017 hajanilipa na ndo kwanza akinitext ananiambia naomba hela shogaangu nna hamu ya kuku mxxiiuuuu
 
Dawa ni kuwasamehe! Wakati nasoma kuna dada classmate nilimkopeshaga laki mbili, ila wiki moja baadaye nikaona urafiki wetu umeathirika. Hanichangamkii kama zamani, akiniona anakuwa uncomfortable basi nilichokifanya nikamwambia kuwa ile laki mbili ipotezee wala usirudishe nimekusamehe.
Since then nimejifunza. Mtu akiwa na shida ni bora nimsaidie nusu ya ile pesa bure kuliko kumkopesha yote.
 
ukiona hivyo ujue they where not real friends,mimi kuna jamaa yangu kwa jinsi tunavyo sitirianaga na kusaidiana,nilikuwama ghafla,nikamkopa laki 4,sasa muda ambao nilisema ntamrudishia,kuna mambo yakawa hayajawa poa,nkawa na laki 2 tu laki mbili nyingie nilihakikiasha na fight mpaka naipata na nikamrudishia,mtu anayekuazima elfu hamsini tuu,achilia mbali laki,usawa huu wa uncle Magu,mshike kwa mikono miwili,huyo ni zaidi ya rafiki na ndugu yako,hivi umewahi kwama shida yako kwa kushindwa elfu kumi tuu? may be umekwama sehemu nk alfu kila unaye mgusa,anakutolea mbavuni,alafu unampata mtu anakusitiri then unazingua
 
bora ya huyo aliyekudhulumu lakini amejali urafiki wenu
 
Ukiona watu wanakopa kwako au wanajenga interest ya kukopa kwako ujue una advantage.

Maana yake kama mtu anakopa kwako laki 5 na unatoa bila shida, basi wewe una uwezo wa kukopa kwa mtu mwingine m5.

Conclusion: Pale yule wa laki5 anaposhindwa kukulipa, wewe utajilipa kwa business utakayofanya kwa ile m5. Walionielewa wanyoshe mikono juu
 
Post yako imenifikirisha sana.
 
Halafu kwa nini mada kama hii umeileta jukaa la Chit chat au unatutania Mkuu.
 
Yaani wewe unafanana na.mimi kabisa sipendi madeni aisee na nikopen na ikatokea nimepata hela naenda kufuta madeni ya watu.
 
Pole sana, kumbe hukujua hilo, sio rafiki tu hata undugu utetereka
 
Yaani wewe unafanana na.mimi kabisa sipendi madeni aisee na nikopen na ikatokea nimepata hela naenda kufuta madeni ya watu.
Madeni yanakosesha raha sana. Na tatizo la wengi anakopa alafu hafanyi kitu cha maana ndio maana wanakua wagumu kulipa.
 
Wakopeshaji wengine mpaka kuroga pia wanaroga ili wakopaji wasisepe kimamae
 
Mimi nimewakopesha rafiki zangu wawili Kila mmoja na wakati wake.

October 2014 Jamaa yangu nilimkopesha Milioni moja taslimu. Alikuwa amekwama ktk biashara yake ya miti ya mbao. Hajanilipa mpaka 26/01/2018 saa 13:24 na cmu yangu hapokei. Nikibadili Namba akipokea akijua Mimi anakata simu.

November 2014 nilimkopesha Jamaa yangu mwingine Milioni 2 taslimu. January 2015 alinilipa Milioni moja, ikabaki moja mpaka Leo 26/01/2018, saa 13:30 hajamalizia. Nikimfuata ananipa jibu cjapata Pesa mkuu.

NB: Wote nimeandikishana nao kwa mwanasheria wangu ambae n rafiki yangu.
 
Mtu akikopa mdai tu, hakuna jinsi. Na kama alikopa kwa siri wewe nenda kamdai nyumbani kwake ili na mkewe ajue kwamba kuna pesa ilikopwa lakini haikufika home. Liwe fundisho kwa wengine wenye tabia hiyo
 
Bora huyo wa pili
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…