Ajira! Ajira! Ajira! Nimekuita mara tatu kwa maana umekuwa hafifu katika mboni za macho ya vijana wengi. Nikikumbuka wosia tofauti za babu na wazazi wangu, kichwa kinazidi kuchanganya zaidi huku nikitafakari maana yao ilikuwa ipi. Namkumbuka pia mwalimu wangu wa Kemia na Baiolojia yule wa kujiita THE DOCTOR kila siku alinambia “ mdogo wangu, Soma sana upate kazi nzuri nina uhakika utapiga sana hela.” Dunia imekuwa duara zaidi ya ilivyokuwa awali kwakuwa, imeongeza pembe katika ukingo wa mstari wa ikweta. Silaumu kwakuwa ukiona gari limelalia Mashariki lazima uende nalo ili uweze kuweka mkao wako sawa. Ndivyo ilivyo katika dunia ya sasa! Usipobadilika na dunia inavyoenda basi utakalia kulaumu kila siku huku ukijua kuwa, lawama zako haziwezi kuongeza chochote katika mfuko wako.
Unajua Nini? Ajira hakuna ndio sote tunajua hilo lakini Je, si una kompyuta na simu? Unavitumia kufanyia nini? Au ndo unatumia kuangalia ‘connections’ kama isemavyo misemo ya vijana wengi wa hapa ‘town’? Haya sasa unataka mchongo? Huu sio ule wa ‘weka kiasi kadhaa na utafute wenzako wawili upate zaidi ndani ya siku fulani’. Unapigwa mchana! Suti kali, ushirikiano wao kwa sana, ila mwisho wa siku tunagombania sote mihogo kwa ‘mama mihogo’ kila siku ifikapo jioni.
Huwa najiuliza maswali mengi, nataka mtaji halafu natoa kwanza nilichonacho ili nikipate kwa watu ambao wapo kwenye kiwango sawa kiuchumi na mimi na cha kushangaza, nipate zaidi ya kile nilitochotoa kwao? Kweli? Changanya zako! Ukitaka kuwa na mawazo chanya lazima ukae karibu na watu wenye mlengo huo. Huwezi kuwa tajiri kwa kukaa na mawazo ya kimaskini muda wote. Enewei, Nilitaka nikupe mchongo wa kutumia sayansi na teknolojia yani simu na kompyuta yako kujiongezea kipato. Tiririka na mimi!
Hivi unajua kuajiriwa sio mpaka ukae kwenye ofisi ya kampuni fulani? Unashangaa nini! Zipo aina nyingi za ofisi kama vile ofisi za nyumbani “home office’ na zile unazojua na kutafuta kila siku. Wapo watu wengi wanafanya kazi na kampuni au taasisi za nje ya nchi wakati wapo hapa nchini. Wanatumia simu zao na komputa zao kutekeleza majukumu yao ya kiofisi wakiwa nje ya ofisi ya kampuni au taasisi zao. Wapo wafasiri na wakalimani huria ‘Freelance translators and interpreters’, waandishi huria ‘Freelance writer’, walimu huria ‘freelance teachers’ na wengine wengi ambao hufanya kazi zao bila hata kufika makao makuu ya kampuni husika lakini, wanajiingzia kipato kila iitwapo leo. Unaweza kuangalia michongo kama hii kwenye tovuti mbalimbali kama; freelany, upwork, freelancer na nyinginezo nyingi.
Kama hiyo haitoshi Je, unatambua kuwa tovuti ‘website’ na mitandao ya kijamii ni mojawapo ya chanzo cha kipato? Tatizo lako unakimbilia kuangalia umbea na mambo mengine ambayo hayana maana alafu unalalamika huna mtaji. Sasa nakwambia tovuti na mitandao ya kijamii kama Instagram, tiktok na mitandao mingine inaweza kukuingizia kipato hata kuliko kuajiriwa. Kwenye tuvuti na mitandao ya kijamii, kadiri unavyopata watembeleaji na watazamaji wengi wa machapisho na video unazoshiriki kila siku ndivyo unavyopiga hela. Inaweza kuwa ngumu mwanzoni lakini kadri unavyozidi kwenda mbele utaelewa somo. Mara moja moja muulize hata Millard Ayo, Haji Manara, Simba sc, Yanga sc, Joel Nnauka, Azam sc na wengineo wanaingiza kiasi gani kupitia mitandao yao ya kijamii.
Unataka mchongo mwingine? Sawa! Kuna hili la kuwashauri warembo mtandaoni. Kama unavyojua, wanawake wengi hutamani kuwa warembo mara zote na hilo halipingiki. Hata wale wenye sura kama yangu bado wanataka kuvutia tu! Ukitaka kumuibia mwanamke mpe ushauri wa kuongeza urembo wake tu basi. Hivi unajua kwanini wale ndugu zetu wanaofanya kazi za kuongeza ‘hips’ wanapiga sana hela? Fikiria hata kwa dakika 5 utapata majibu. Kwa hiyo, muda mwingi wanawake hukaa mtandaoni ili kujua jinsi ya kufanya miili yao ivutie watu wanaowazunguka na hata wapenzi wao. Sasa, kuanzisha mafunzo ya mtandaoni ya jinsi ya kufanya mwili kuvutia kunaweza kukuongezea mapato ya haraka ukiwa nyumbani tena kwa kutumia simu au komputa yako.
Isitoshe, sio wanawake tu bali wapo wanaume wenzangu na mimi wanaotamani kuwa na miili mizuri kwa lugha ya nyumani ‘Sixpack’. We tambua kuwa, kozi za mkondoni/mtandaoni zinaweza kukufanya upate pesa nyingi kupitia hitaji lao la kutengeneza miili.
Ngoja niongeze la ziada, tunajua kuwa umesoma sana ndio lakini Je, unajua kuwa watu wanapiga hela sana kupitia uandishi wa wasifu wa watu (CV/Resume writing). Liweke kwenye akiri yako sasa! Uandishi wa wasifu umekuwa kazi muhimu kwa wataalamu wenye uzoefu katika tasnia hii. Wasomi na watu wenye pesa hujikuta wamenaswa katika mtego wa ukosefu wa wasifu mzuri na zenye kuvutia waajiri. Kwa hivyo, ikiwa wewe ni mwandishi mzuri wa wasifu, unaweza kupata mapato ya kutosha nyumbani kwako, umenyoosha miguu juu na juisi yako pembeni huku ukiandika wasifu mbalimbali za watu tofauti ulimwenguni. Uzuri wake ni kuwa hata kama una kiduka chako cha matunda bado utaendelea kupiga zako hiyo pesa tu
Kalamu yangu koma! Tena koma kabisa! Mtu asipotaka kukuelewa hata kama utasema nini bado atatafuta sababu ya msingi kujilinda ilimradi tu apate sehemu ya kusimamia na kukupinga. Kuna mtu mwingine amewaza eti ‘hivi huyu anayesema haya yeye ameingiza kiasi gani kupitia haya anayotwambia?’ Unataka kujua nimeingiza kiasi gani? Sawa! Hivi ushawahi kuongea na mlevi kuhusu madhara ya ulevi? Mvuta sigara je? Babu yangu alinambia “Vijana mkifika vyuo vikuu mnahisi ndo mnajua kila kitu. Nilianza kuvuta sigara nikiwa na mika 17, nikaoa na mpaka nikamzaa baba yako halafu leo unasema ati sigara inaharibu mapafu? Hayo mapafu yangetaka kuharibika, si yangeharibika hata kabla sijazaa? Kwani si unaona mpaka sasa nina afya nzuri sana? Ningekuwa na mpafu yalihoharibika ningemzaa baba yako?” Lakini, wakati akiwa anaendelea kuongea nikasikia Koh! Kho! Kho! Puuuuh! Akakohoa na kutoa kikohozi kizito sana. Sikutaka kupoteza muda nami nikasema ngoja nipotee zangu. Tangia siku hiyo sijawahi hata kuongea naye kuhusu madhara ya sigara na pombe.

Upvote
1