mwakajumba1
New Member
- Aug 9, 2022
- 3
- 1
Chakula, malazi na makazi ni mahitaji ambayo kila mwanadamu lazima ayapate kila, ndio maana yamewekwa katika mahitaji ya msingi ya mwanadamu. Kila siku mwanadamu anapambana ili kuhakikisha anakua na uhakika wa nini atakula, nini atavaa na wapi atalala.
Kabla ya kufikiria ubora wa mahitaji haya lazima mtu awe na uhakika wa kuyapata kwanza. Mfano, mtu akishajua ana uwezo wa kuvaa ndipo atakapofikilia avae vazi la aina gani. Mwanadamu analazimika kujishughulisha na shughuli mbalimbali ili kweza kuyapata mahitaji hayo matatu kila siku.
Wakati mtu anafanya jambo fulani ili aweze kujipatia mahitaji hayo,matokeo ya kile anachokifanya kinawasaidia wengne kujipatia mahitaji yao ya msingi pia. Mfano, wakati mkulima anaandaa mazao yake, yeye atapata chakula lakini pia anaweza kuyauza kwa mtu anaehitaji chakula na akapata pesa itakayomsaidia kuboresha malazi na mavazi yake.
Kwa maana hiyo inahitajika ufahamu maalumu katika jambo fulani ili kumuwezesha mtu kujipatia mahitaji ya msingi ya kila siku. Hapo ndipo linapokuja suala la elimu, ambayo inaweza kuwa rasmi au siyo rasmi. Elimu isiyo rasmi imekuwa ikiendeshwa na jamii zetu hata kabla ya ujio wa wakoloni ambao walipofika wakaanzisha mfumo wa elimu rasmi. Bila kujali aina ya elimu (iwe rasmi au isiyo rasmi) lengo kuu ni kumpatia muhusika anaejifunza (mwanafunzi) uwezo wa kufanya shughuli zitakazomuwezesha kujipatia mahitaji ya msingi ya kila siku.
Mamlaka zinazosimamia mfumo wa elimu rasmi zimejitahidi sana kuielimisha jamii umuhimu wa mfumo huo na zimejitahidi kuwekeza katika mfumo huo ikiwa ni pamoja na kuandaa mazingira ya kuwezesha mfumo huo kwa kujenga shule, kuleta vifaa vya kufundishia na kujifunzia pamoja na kuandaa wataalamu (walimu) kwa ajili ya kutoa elimu rasmi.
Hivi karibuni kumekua na idadi kubwa sana ya wahitimu wa mfumo rasmi wa elimu, na pia kumekua na ongezeko kubwa la taasisi zinazojihusisha na kuhudumia jamii kwa mfumo huu rasmi wa elimu (taasisi za serikali na zisizo za serikali). Ongezeko hili ni ishara kuwa jamii imetoa mwitikio chanya kwenye mfumo rasmi wa elimu.
Kilichonisukuma kuandika hapa ni vile tatizo la ajira linavozidi kuongezeka kadiri wahitimu wanavoongezeka. Ni kweli mfumo rasmi wa elimu una0tumika katika nchi yetu unampa mwanafunzi ufahamu wa namna ya kutekeleza jambo fulani( kutegemea na kada anayosoma) lakini ufahamu huo anaoupata unatakiwa akautumie katika maeneo ambayo yameandaliwa rasmi ili kuruhusu ufahamu huo kutumika.
Mfano, kama mtu anasoma ualimu basi alichosoma kitamsaidia pale tu atakapopata ajira kwenye shule. Lakini kwa bahati mbaya huko shule tunakosoma, hakuna somo linalofundisha namna ya mtu kuanzisha shule, ili yule anaesoma ualimu atakapomaliza akute tayari kuna uhitaji wa walimu.Mfumo wetu wa elimu umejikita sana kwenye kuzalisha waajiriwa lakini hakuna namna iliyo rasmi inayomfundisha mtu kujiajiri au kuajiri wengine.
Wakati mfumo huu unaanza kulikua na uhitaji wa wataalamu katika kada mbalimbali,ndio maana mamlaka husika zikatilia mkazo sana kuzalisha watu wenye ujuzi kulingana na uhitaji lakini wenye kuweza kuajiriwa maana kipindi hicho waajiriwa walikua wanahitajika sana.
Ilikua inafahamika kuwa mtu akipata ajira,mathalani serikalini, uhakika wa kujipatia mahitaji yake ya kila siku ya msingi unakua mkubwa sana, hali hii ilipelekea watu wengi ambao hawakupata elimu rasmi kipindi hicho kuamini ugumu wa maisha wanaopitia ni kwakua wamekosa elimu hiyo.
Muamko ukaongezeka kwa jamii kuhusiana na mfumo huo wa elimu na kupelekea wazazi na walezi wengi kupeleka watoto wao shule, lengo kubwa ni kuhakikisha wanapata ujuzi utakaowawezesha kuajiriwa, ikafika mahali watu wakaanza kuchagua aina fulani ya kada kwakua zilikua na uhitaji hivyo kupelekea kila anaehitimu kupata ajira ya moja kwa moja. Hali hii ikapelekea hata kuongezeka kwa shule na vyuo katika jamii ili kuongeza idadi ya wahitimu (ambao wameandaliwa kuajiriwa).
Sasa ongezeko la tatizo la ajira ni kwasababu jamii imepokea vizuri mfumo wa elimu ambao ulipendekezwa na mamlaka husika, lakini kinachotokea ni mfumo huo kuanza kuelemewa. Ni mara nyingi imekua ikisikika "vijana wasitegemee kuajiriwa, wajiajiri" lakini ukiangalia ujuzi aliopewa wakati yuko shule ( takribani miaka 16 na zaidi) haumuoneshi namna ya kujiajiri.
Mfano leo hii mtu anasoma udaktari wa kutibu binadamu ili akafanye kazi katika taasisi yenye miundombinu ya kukidhi ujuzi alionao, alafu anahitimu anaambiwa akajiajiri? Atawezaje?
Mamlaka husika zinatakiwa kujua kuwa, mfumo wa elimu tulionao ni kweli ulitusaidia kwa kipindi fulani, lakini sasa umekua chanzo cha matatizo na sio suluhu kama ilivyokusudiwa.
Sio kila njia inaweza kukusaidia kila wakati, kwa maana njia fulani inaweza kuwa nzuri kwa kipindi fulani tu,lakini kwenye kipindi kingine ikawa haina msaada, au hata ikawa chanzo cha matatizo. Hivo ni vizuri kubadili njia za kutatua matatizo kuendana na hali ilivo sasa.
Hatua ya kushawishi jamii ipokee mfumo wa elimu rasmi imefanikiwa, inatakiwa sasa mamlaka husika zianze kuangalia huo mfumo ambao umepokelewa na jamii unatatua matatizo ya jamii au ndio unaongeza matatizo.
Ni vizuri kukawa na elimu inayomuwezesha mtu kuweza kuzalisha ajira,kuliko kufikiria kuzalishiwa ajira ili aajiriwe. Elimu itakayomsaidia mwanafunzi kuangalia uhitaji uliopo katika jamii na kuweza kutatua uhitaji huo huku yeye pia akinufaika na anachokifanya.
Hivi sasa muamko wa wanafunzi ambao bado wanasoma, hasa ngazi ya vyuo umekua mdogo sana baada ya kuona wale waliowatangulia wakiendelea kujazana mtaani bila kuwa na kile ambacho waliamini kwa kupitia elimu aliyoipata wangekuanacho.
Inafika kipindi mtu kasoma mpaka chuo kikuu,lakini kwa kukosa ajira analazimika kufanya shughuli ambayo inahitaji ujuzi wa kujua kusoma,kuandika na kuhesabu tu, ujuzi ambao aliupata toka akiwa darasa la kwanza. Yani mtu anatumia miaka 16 shule ili aje kutumia ujuzi alioupata miaka 14 iliyopita.
Mfano, siku hizi kuwakuta wahitimu wa vyuo vikuu wakiendesha bajaji na bodaboda imekua sio jambo la kushtua. Hii inapelekea hamasa kwa jamii kupungua, na kama hatua za haraka hazitachukuliwa, miaka ya huko mbele nchi itajikuta inakosa wataalam kabisa na kuanza upya kupambana na jamii kuhusu suala la elimu rasmi.
Kuendelea kutoa elimu yenye lengo la kuzalisha wataalamu wa kuajiriwa tu huku mahitaji ya waajiriwa yanapungua ni kusababisha mfumo wa elimu rasmi kuanza kupoteza maana yake halisi na kupelekea jamii kuanza kuukwepa.
Ni rai yangu kwa mamlaka zinazohusika, kupitia upya mtaala wa elimu unaotumika nchini ili kurekebishwa kuendana na mahitaji ya jamii kwa sasa. Na jambo hili liwe endelevu maana teknolojia inabadilika na kukua kila siku.

Upvote
0