KERO Ukosefu wa maji Kata ya Buhembe - Manispaa ya Bukoba unatuumiza wengi

KERO Ukosefu wa maji Kata ya Buhembe - Manispaa ya Bukoba unatuumiza wengi

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Sisi Wakazi wa Kata ya Buhembe katika Manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera tunaomba Mamlaka ya Maji Bukoba (BUWASA) kushughulikia suala la ukosefu wa maji kwenye Kata ya Buhembe.

Serikali imewekeza fedha nyingi ujenzi wa tenki kubwa la maji katika Kata ya Buhembe na limeshazinduliwa na Mwenge wa Uhuru tangu Mwaka 2024 lakini Wananchi wa Kata hiyo na Kata jirani hatuoni faida ya tenki hilo lililogharimu fedha nyingi za Wananchi.

Mamlaka husika itoe majibu na itatue tatizo hilo, tunaoumia ni wengi.
461686936_911899590989055_132373765208861869_n.jpg

461610569_911846614327686_5448977760230892651_n.jpg

461710472_911846634327684_3047989560563348196_n.jpg
 
Back
Top Bottom