A
Anonymous
Guest
Katika nchi yetu kuna baadhi ya maeneo kupata huduma mbalimbali za msingi kama maji, umeme n k imekuwa kawaida sana, lakini hii hali imekuwa tofauti sana katika halmashauri ya Mbulu mji hasa maeneo baadhi ya vitongoji hasa kitongoji cha Nyangera Kijiji Cha Jaranjar, na watu wanachota kwa kutumia punda kwa sababu ya umbali wa maji. Yaani mtu anatoka saa 12 asubuhi kurudi saa tatu nyumbani.
Je, ni lini Serikali itayaangaza maeneo haya kupatiwa maji safi na salama? Tunaomba Mbunge wetu pamoja na diwani hili linawahusu kutolea majibu. Kuchota maji kwa kutumia punda kiukweli ni zama za zamani sana.
Naomba kuwasilisha