KERO Ukosefu wa maji zaidi ya mwezi mmoja Tabata

KERO Ukosefu wa maji zaidi ya mwezi mmoja Tabata

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Insidious

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2020
Posts
654
Reaction score
895
Kwenu Wahusika,

Naandika kutoa malalamiko yangu na kuhusu kukosekana kwa maji kutoka DAWASA katika maeneo mengi ya Tabata, kwa zaidi ya mwezi mmoja sasa ambayo pia inatufanya kuingia gharama kubwa kupata maji hayo. Bill yetu ya hivi karibuni inaonyesha matumizi ya maji kuwa sifuri, ikionyesha kuwa hakuna maji yaliyotolewa.

Hata baada ya kupiga simu kwa huduma kwa wateja, tulijulishwa kwamba hawana taarifa kuhusu tatizo hili na hawawezi kutoa maelezo yoyote. Kukosekana kwa mawasiliano na uwazi huu hakukubaliki.

Soma Pia:
Tunahitaji kwa haraka ufafanuzi kuhusu hatua zitakazochukuliwa kutatua tatizo hili. Ikiwa kuna mpango wa mgawo wa maji unaoathiri usambazaji wetu, kinapaswa kutangazwa hadharani ili wakazi wote tuweze kujipanga kikamilifu.

Tumechoka na hali hii na tunatarajia suluhisho la haraka.

IMG_0380.jpeg
 
Back
Top Bottom