Ukraine imekubali kuipa Marekani madini yake yenye thamani ya $500B

Ukraine imekubali kuipa Marekani madini yake yenye thamani ya $500B

hamis77

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2013
Posts
13,628
Reaction score
20,992
Ukraine imekubali kuipa Marekani madini yake yenye thamani ya $500B

Moscow imepiga kelele isiyo na madhara

Ulaya imefuata nyayo za Trump

Marekani hadi muda huu imetumia $183 B kama msaada wa kivita kwa Ukraine dhidi ya Urusi. Ni pesa nyingi sana. Wengi waliuliza, Marekani itapata nini nyuma ya msaada huo?. Sasa imepata mara mbili ya faida kubwa itakayotokana na madini hayo. Pamoja a hilo imepata mashamba ya ngano pamoja na kumiliki viwanda vya mbolea vya Ukraine. Kifupi Ukraine imenunuliwa na Marekani. Zelenky ametoa yote haya ili kubadilishana na msaada wa kijeshi kutoka Marekani. Maana Trump alimwambia ukigoma nampa Putin Ukraine.

Hivyo Trump hana kificho, ukimpa siri Trump ni kama umeamua iwe wazi tu. Ni kweli hakuna msaada wa bure duniani, ukiona mtu anakujali na kukupa misaada jua nyuma ya msaada huo kuna jambo analolihitaji kwako. Bepari yoyote ni mwekezaji, hatoi pesa ya bure. Kila centi yake nyuma yake ina faida usiyoijua.

Daima Marekani ina siri nyingi ambazo washirika wake hawazijui, maana mikataba yake ina siri nzito. Na marais wake wakiwa watu wa siri katika utendaji wao kwajili ya maslahi ya Marekani yaliyofichwa nyuma ya White house. Ila kwa Trump ni vinginevyo. Yeye anaonekana ni mropokaji lakini ukizama ndani utaona anaonesha uhalisi wa USA katika eneo la maslahi.

Ulaya imefuata nyayo za Trump

Toka ameingia madarakani mnamo 21 january, Trump amefunga milango mingi ya misaada hadi nchi zilizokuwa zinasaidiwa, kwamba nazo zitoe faida kwa Marekani kama makubaliano yalivyo. Hata kutishia kuibeba Greenland ni tishio la kuitaka Ulaya iweze kutoa maslahi sawa kwa pande zote ikiwemo uchangiaji katika Nato. Aliwaambia kama mtasita, ataikabidhi Ulaya kwa Putin. Sasa Ulaya nayo imefuata utaratibu wa Trump wa kuongeza bajeti kwenye Nato na kuzuia misaada kwa wasaidiwa ili itolewe kulingana na faida ya upande wa msaidiwa. Hivyo sasa ni wakati wa malipo wa nchi saidiwa kwenda kwa nchi saidizi. Tujipange, huu ni wakati wa mavuno. Na ndio maana Jordan na Misri zimetishiwa kuporomoshewa uchumi wao kama zitaendelea kupinga mpango wa Trump wa kuitwaa Gaza. Maana nazo ni nchi kuu mbili saidiwa kwa upande wa Afrika kaskazini na mashariki ya kati. Hivyo misaada inayomiminika Afrika nyuma yake imebeba faida za mabilioni kwa wahisani (watoaji). Hivyo ardhi na madini na rasilimali zetu ndio rehani ya misaada hii.

Trump hana siri

Sasa ameweka wazi kilicho nyuma ya vita vya Ukrane. Moja wapo ni madini adimu ambayo nusu yake yapo kwenye majimbo ambayo Urusi imeyatwaa. Urusi ilijua moja ya target ya US ni madini yaliyopo Donbas. Hivyo Urusi ikaenda hapo haraka kwa kivuli cha kuwaokoa watu wa Donbas kwamba wanaonewa na serikali ya Zelenky. Hivyo vita vya ulimwengu huu kiini chake ni "maslahi". Trump naye amejitwalia sehemu kubwa ya nchi ya Ukraine yenye 80% huku Urusi akiwa na 20%. Hivyo Urusi imepiga kelele ikiilaumu Marekani kutwaa madini ya Ukraine pamoja na hilo kuifanya Ukraine kama hub ya gesi na mafuta kwenda Ulaya. Urusi nayo imetatizwa, aidha ichague kuendelea na vita au kuachiwa ardhi ya Ukraine iliyotwaa na vita vikome. Wapo njia panda ingawa wameonesha kulegea. Hivyo wakikubali ni dhahiri Marekani na Urusi wataendelea kuwa majirani. Hivyo Urusi haitaweza tena kumuondoa Marekani hapo Balkan.

Trump amejivuna kwamba ameshaongea na Putin na Zelenky na wamekubaliana. Hivyo meza ya mazungumzo ya amani msingi wake mkuu ni kuigawa Ukraine huku mfaidika mkubwa ni Marekani. Huku Urusi akiachwa akiwa na majeraha makubwa ya vita na vifo vya malaki ya wanajeshi wake. Huenda atajilipa kwa madini ya Donbas aliyoyapata kwa jasho na damu. Hivyo kelele za Moscow hazina madhara tena kwa Marekani.
20250207_212308.jpg

Na Jeff
 
Zelensky hajasaini bado anataka guarantee ya ulinzi dhidi ya Russia

Screenshot_20250214_130828_Chrome.jpg
Screenshot_20250214_130913_Chrome.jpg
 
Back
Top Bottom